MSANII WA PWANI AINGIA BONGO NA KUPIGA BONGE LA COLLABO NA MZEE YUSUF MWENYEWE!!!!!
Wengi wanamfahamu kama Single Jay,msanii anayetokea kusini mwa pwani. Single-Jay au ukipenda Jizze ni msanii anayefanya muziki wa hiphop na afrofusion.Jay alisikika kwa mara ya kwanza kwa wimbo MAMA uliofanya vizuri Japo sio sana. Mshikaji huyu alisafiri bongo kufanya collabo na wasanii wa huko waliomuita kufanya kazi naye.
Kufika bongo wasanii aliokuwa afanye kazi nao walikuwa bize kidogo kwa hio Single Jay ikabidi aingie studio ya C9 na kufanya muziki peke yake. Jay alieleza hivi...
"Washikaji wenyewe wa bongo wanajiita Kaka chotara,Steve Ghostwritter, Superboy na Kissy music.Hao ndio washikaji tulio organise hio kollabo na kusudi ya kollabo nikusambaza mziki wangu sio Kenya pekee tu bali Afrika Mashariki."
PWANI USANII: HIVI JE ILITOKEAJE UKAPIGA COLLABO NA MZEE YUSUF???
SINGLE JAY:Wasanii hao wa Bongo walitaka niende tufanye ngoma ila bahati mbaya nilipofika wakawa wengine wameshikika kiasi sasa ikabidi tuondoe hio issue ila nikaona nikirudi bila kufanya ngoma nitakua nimeenda hasara ndio nikaamua kwenda kwa c9 kufanya mambo.Nilipofika kwa c9 bahati nzuri Mzee Yusuf alikuepo pia.Nikaongea na Baba Kash pale akaniombea kollabo na Mzee Yusuf hakupinga,basi tukafanya kazi."
PWANI USANII: JE KIKOSI CHAKO CHA LAMINI3 BADO KIPO??
SINGLE JAY:Kuhusu LAMINI3.Kikosi chetu bado kipo na tupo imara kabisa na mziki sema tu kila mmoja yupo bize sana ila kuna siku huwa tunakutana tunaongea kuhusu mziki.
PWANI USANII: KWA SASA KANDO NA COLLABO HIZO.UNA PROJECT ZIPI TENA ULIZOTAYARISHA??
SINGLE JAY:Kando na hio ya Mzee Yusuf.Kuna kollabo nimefanya na kigoto.Halafu kuna solo project nimefanya mk2 studios.So mashabiki kazi zipo nyingi zinakuja.
Comments
Post a Comment