TOP 8:RECORDING STUDIO NANE KALI PWANI

8.MK2 STUDIO-Kutana na produza Plion na Magustu babu ambao kila uchao wanaleta vipaji vipya.Jay kiny,Alkenia Luv,Wawindaji ni baadhi ya wasanii waliofanya na wanaofanya kazi MK2. 
7.TEE HITS.Bila shaka hakuna pingamizi kuwa produza Tee single-handedly bila usaidizi wowote ameifikisha studio yake mbali.Amemkuza Dazla,Double-k na kwa sasa Mynas vilevile Fat-s,kidis,Ali b wote washafanya kazi na produza Tee. 
6.SQ RECORDZ-Studio hii chini ya mbawa zake Produza Ammz Jadidi imeshikilia sanaa ya pwani kwa sana.Ammz aliyechaguliwa kama producer of the year kwa coast awards 2013 alimleta ,kaa la moto,luvmums na wengineo.Tusisahau wimbo wa Subiri by coast all stars. 
5.THUNDERSOUND RECORDS. Produza Morbiz almaarufu Sheriff ndiye mlezi wa vipaji vingi hapa pwani.Maproduza kama Tee,Gogolow,Tk2,Amz,andahwotah,Kicksgonga na wengineo walipitia kwa Morbiz.Wasanii vilevile kama Chikuzee,Rojo-Mo,Dazlah,CLD,Fat-S,Tiera G,Susumila na wengine wengi walipitia kwa Morbiz na kwa sasa Xmathare,Sultan wa Pwani,Sudi Manjewa ni baadhi ya wasanii wanaofanya vyema chini ya Thundersound. 
Produza Morbiz



 4.KELELE RECORDS .Hii ndio headquaters ya marapper na dancehall artistes wote wanaotamba kwa sasa.Sema,Johny Skani,Ohm's Law montana,Odinareh,Kassamoney tuendelee ama.....? Studio ambayo imetoa riddims zinazochezwa international,eg Sheshe riddim.Producer Teknixx anahitaji hongera. 
3.CRACKSOUND RECORDS. Kilifornia ndio kuleeeeee.......!!! Tunasafiri mpaka Kilifi kupatana na mfalme Jay Crak aliyewaleta Escobar babake,Shaa biggy,Mchafuzi wa mapozi,LaiLai,Susumila na wengine wengi.Wengi wao wanamuita mfalme wa hiphop pwani, Jay-Crak. 
 2.JUNGLE MASTERS PRODUCTION. Dogo Richy,Majid,Lypso,Harsh B,Calvo wakali wote wa muziki wa maloveydovey wapo ndani ya nyumba ya mshale bora almaarufu Produza Emmy Dee.Top chart za pwani huwezi kosa muziki wa Jungle masters na bila shaka tumalizie kwa kuwapa heko Prince Audio na Jos-k madala. 
Produza Emmy Dee

1.HORNET RECORDZ Producer Tk2 aliipatia tuzo studio hii mwaka jana kwa coast awards na vilevile nyimbo kalikali kama kichapo cha mapenzi ya kigoto,kibebe ya chikuzee,ngoma itambae,bachelor,rambirambi za susumila zote zaongoza chart za pwani.Hornet records kweli imefanya bidii na kwa mwaka mmoja tu imechukua sanaa ya pwani kwa anga zingine.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA