KUTANA NA SKILL-T VOLCANO



P.U:TUAMBIE JINA LAKO HALISI NA LA USANII 
A:Stage name ni Skill-T Volcano na langu halisi ni Liston Tumaini.
P.U:ULIANZA MUZIKI LINI?
A: Nilianza mziki 2005 chini ya producer Saint-P pamoja na U.n.d.a ndani ya Onepath recordz.
P.U:USHAFANYA KAZI NA RECORDING STUDIO ZIPI?  
A:Niliwahi kufanya kazi na studio kama vile Greenhouse,Boomba recordz na kelele recordz.
P.U:UNA BIDII KWELI,ENHE TUELEZE ZAIDI.
A: Kwa hivi sasa niko na ujio mpya ambao nilifanya na producer Techqnics kutoka Kelele recordz natayari nishaichia kwa radio station kadhaa kama vile pwani fm na nyinginezo. 
P.U:PROJECTS ZIPI ZA MUZIKI ,WAJISHUGHULISHA NAZO KWA SASA? 
A:Kwa sasa nafanya kazi na MYDG MUSIC 4 PEACE ambayo ni group ya wasanii inayo deal na awareness juu ya PEACE iliyosajili wasanii kama Skill T, Cox na Mck'zoo na wengineo. 
P.U:KWENYE KUNDI LENU JE MSHAFANYA MUZIKI KWA PAMOJA? 
A:Tulifanya album ya AMANI KENYA chini ya KTI, USAID KENYA. 
P.U:UNA NDOTO NA MATUMAINI GANI KIMUZIKI? 
A:Ndoto yangu kimziki ni kuhakikisha kuwa mziki wa pwani uzidi kukua ili kuona jamii inaelimika nakuwajibika vilevile kwangu mimi kama skill T mziki ubaki kua kitega uchumi iliniweze kutimiza malengo nakuwakilisha ndoto kikamilifu.
P.U: SASA NATAKA TUONGELEE KUHUSU WEWE KAMA MUIGIZAJI. ULIPATA NAFASI VIPI KUIGIZA KWENYE KIPINDI CHA MOMBASATI? 
A:Nilipata hii chance kupitia my Talent through M.Y.D.G.(MALINDI YOUTH DEVELOPMENT GROUP) Ambayo ni Community based Organization ambayo inadeal na sanaa mjini Malindi. Wahusika wa kipindi na wasimamizi wa kipindi walikuja Malindi wakasearch Talent na Audition ikafanyika.
P.U:HALAFU,LIPI LILIFUATA? 
A: Nashukuru napatikana katika kipindi cha Mombasati kwenye QTV!!!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA