PRODUZA MWENYE UMRI MDOGO PWANI// Petrooz ni
produza wa muziki anayetokea papa hapa jijini Mombasa.Gwiji huyu mwenye
umri wa miaka kumi na tisa alianza kuandaa muziki tangu alipokuwa shule
ya upili.Petrooz aliunda beat na kuziuza huku akirekodi muziki na
kujilipia karo ya shule.Kwa sasa yupo na track mpya aliyowaandalia
Hustla jay na Fikra teule inakuja hivi karibuni.
MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.
Ni msanii aliyekubalika na wengi na aliyevuma kwa vibao motomoto kama; mtoto wa shule,umaskini si kilema,kadem,toka nenda,kadem kameparara na nyinginezo. Msanii huyu aliyemaliza shule ya upili mwaka uliopita alifuzu na kuchaguliwa kwenye kikosi cha askari polisi kitengo cha AP. Ranny aliyekuwa studio ya Homeworks na kuhamia studio ya Mwamba records kwa sasa yupo kwenye kambi mafunzoni na aliahidi kuwa kamwe hatowacha muziki,atashughulika na muziki pamoja na kazi yake mpya ya kulinda usalama.
Comments
Post a Comment