PRESENTER TEDDY MWANAMGAMBO ATOA USHAURI KWA WASANII
Hili ni swali ambalo wasanii wengi wanaoanza safari yao ya kimziki wameniuliza mara nyingi. Wenye jibu sahihi la swali hili inafaa iwe wasanii wakubwa ambao tayari wamefanikiwa kupata idadi kubwa ya mashabiki. Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kugundua kwamba wasanii hawa wameekeza juhudi nyingi katika kulinda siri hii ya mafanikio.
Hakuna msanii mkubwa ambaye huwa tayari kufichua siri yake ya mafanikio, hususan katika kukuza idadi ya mashabiki, jambo ambalo huwaacha wasanii wadogo wanaoanza mziki wakitapatapa na mwishowe kufanya makosa mengi ambayo yanaweza kuepukika iwapo wasanii wakubwa wangeshirikiana katika kukuza vipaji vipya katika tasnia.
Wivu wa maendeleo umetawala mioyo ya wasanii wengi wakubwa ambao wewe kama msanii mdogo ukikutana nao watakuchekea ukizungumza nao na kukuponda unapo wapa kishogo.
Ijapokuwa hakuna utaratibu rasmi wa jinsi ya kukuza idadi ya mashabiki.Kupitia miaka ya kadhaa ya kutazama kukua kwa tasnia ya mziki wa kizazi kipya kanda ya pwani, labda mtazamo wagu unaweza kukupa inshara ya lilipo jibu iwapo hutapata jibu katika huu mtazamo wangu.
1. BIDHAA.
Ukitaka wateja lazima uwe na biashara/duka na bidhaa zinazovutia wengi. Msanii anayetaka mashabiki wengi lazima awe na bidhaa itakayovutia mashabiki mithili ya maua kwa nyuki. Lazima iwepo sababu kuu yakuwafanya watu wanaoskiza wasanii mbali mbali,kukupenda wewe zaidi badala ya wasanii wengine.
Bidhaa ninayo zungumzia hapa ni mziki. Mziki wako unafaa kuwa mzuri na mtamu maskioni mwa wateja, ili uwanase na wagande katika kazi zako kila unapoachilia wimbo.
Lazima uwe na historia nzuri ya kimziki .Hapa namaanisha, ngoma tamu mbili au tatu zinazofuatana zinatosha kuanzisha vuguvugu la watu wanaoshabikia mziki wako.Sio ngoma mmoja kali halafu ya pili na ya tatu mbovu; ya nne kali tano mbaya! No ….hii inawavunja moyo wanaokufuatilia. Nitajie mziki mbovu unao weza kuhusishwa na msanii mkubwa Afrika Mashariri Diamond?
Kama ngoma yako ni mbovu (hata kolabo), haina haja itoke. Si lazima, wala si sheria ngoma isambazwe kila mastering inapokamilika studio.
Skiza, tafta ushauri kwa wengine wanaojua mziki na soko ili wakusaidie katika kuchuja mziki unaotoka, ili kuhakikisha ni mzuri.Unaeza husisha magwiji kadhaa wa kimziki unaoamini watakupa ukweli kuhusu quality ya ngoma hata presenter wanaokwambia Ukweli. Hata hivyo jihadhari na wale wafisadi waanaokuchocha utoe ngoma mpya, wakijua utawapa hela za promo na interview katika stesheni zao.
2. ANDAA MATAMASHA.
Ukifikisha nyimbo kadhaa ambazo unadhani zinaweza kuwatumbuiza mashabiki anza kujishughulisha na maswala ya kupiga show. Hii haimanishi ukiwa na ngoma moja lazima upige show pekeyako. unaeza kufanya kolabo na mwengine ambaye atafanya show yenu iwe nzuri na kutumbuiza mashabiki kuhakikisha wanapata “value for their money”
Tafuta mikahawa ambayo unadhani utaweza kuandaa show amabazo zitafanikiwa. Ufanisi wa matamasha unayofanya yata convince wengine kuungana na mashabiki wako na kupiga jeki azma yako ya kugeuza revelers kuwa mashabiki wako usiku wa tamasha na kesho asubuhi redioni.
Silazima iwe mkahawa mkubwa unaotambulika na majina makubwa makubwa ya wasanii wanaofika kupiga show.
Hii inasaidia pia kujenga confidence na ku perfect performance skills.
Baadae unaweza kuongeza namba ya show kwa mwezi. Kumbuka juhudi hizi zitahitaji uhakikishe ume perfect mchakato wa kuandaa matamasha.
3. KUJICHANGANYA.
Kujichanganya na wengine wanaofanya show. Siri moja ya mafanikio maishani hata katika maswala mengine, ni kujichanganya na waliofanikiwa ama wanaofanikiwa maishani.Ukijihusisha na ma’failure chances za wewe kuwa failure ziko juu na ukijihusha na achievers bas hata wewe unaurahisi wa kuwa achiever.
Jihusishe na wasanii wakubwa wanaoandaa shows za kufana na achana na wale wa kupiga mdomo kijiweni/studio wanaodai kuwa wasanii wakubwa na hawaskiki wakipiga ma’show. Aidha hakikisha unajihusisha na wengine wanaohusika katika maandalizi ya matamasha aina yako. “Promoters.”Hii inakupa fursa ya kuona kinachoendelea katika matamasha haya na kujua yepi ya kufanya na yepi siyakufanywa ili tamasha lako ukiandaa liweze kufana.
Hii inaweza kuhusisha uandalizi wa matamasha kwa ushirikiano na wengine walio na experience katika haya maswala. Learn from them. kuonekana kwako katika matamasha mbali mbali kunaweza kuongeza mashabiki wako kwani ni wengi watakuona ukiwasilisha kazi zako huku ukiwatumbuiza.
4. TUMIA MTANDAO.
mtando ni njia mpya ya kuwafikia watu wengine na ku socialize nao. Tumia mtando kujenga fan base kwa kuhakikisha visibility ya maisha yako ya kimziki katika mtandao. Jenga jina zuri kwa kuwa muangalifu wa vitu unavyo post katika mitandao ya kijamii. Picha unazosmbaza zinafaa ziwe za kuchangia to your positive publicity. Weka picha za events zako tangaza mpangilio wako wa kimziki interviews etc. Make information about you as an artist readily available to prospective fans in the social media.
5. VITU.
Vitu ambavyo watu wataweza kuvihusisha na mazuri yako ya kimziki. Vitu ambavyo vitawakumbusha kukuhusu wewe kama msanii ama kusambaza ujumbe wa uwepo wa msanii ka wewe katika game. Merchandize inaweza pia kuwa njia moja wap ya kujipatia hela kwa kuuza vitu vyako directly kwa mashabiki ama wanaojaribu kuwa mashabiki wako. vitu hivi vinaweza kuwa T shirts, Bandanas etc.
6.SAMABAZA
Sambaza matamasha yako kati maeneo tofauti. Pole pole baada ya kuandaa matamasha kadhaa ya kufana unakokuwa na fan base kubwa, jaribu kusambaza juhudi zako za kuandaa matamasha katika sehemu zengine amabazo labda si stronghold zako.
Mwanzo unaeza ku kolabo na mwengine ambaye ni stronghold zake kabla ya kuweza kuandaa lako kivyako ugenini.
7.JIHUSISHE
Jihusihe na media house. Be visible. Wacha uonekane kimbelembele katika activity ya media houses. Jichanganye na presenters activity za media houses ambazo zinaleta mashabiki pamoja. Jiulize kwa nini wanasiasa wanashindwa kuacha kupiga siasa mazishini. Labda akifanya mikutano yake hawapati ule umati so hu ana take advantage ya any opportunity ya umati.
Unafaa kuchukua advantage wakakti wowote umati umekusanywa. Media houses zina mvuto wa mashabiki so jipeleke .. ensure your presence is felt. Tumia hiyo nafasi kujipa promo.
Aidha ukaribu na wasikadau kadhaa katika media inakupa advantage ya kupata interview, promo na publicity kwa urahisi.
8.HELA.
Dunia ya sasa bila hela ni vigumu kupenya. Tumia hela panapotakikana utumie. Hela unazopata kutokana na ma show hakikisha una hifadhi kadhaa ili uweze kuzitumia katika mahangaiko ya kimziki.
Ukiwa na hela inakua kama handaki lako katika vita vya kutafta umaarufu. Haina haja utumie hela zote za show ununue pombe usherekee na masela.
Wachache wanapata nafas ya kutengeneza hela kupitia mziki, so ukizipata zitumie poa na usifuje. Invest kati game ka biashara na bila shaka utapata mafanikio, moja wapo kupata mashabiki wengi.
Comments
Post a Comment