MEET OMMY KESSY
Leo tunamhoji msanii anayetokea pande za likoni na aliye na kipaji si haba. Wengi wanamuita 'waziri wa mahaba' kwa sauti yake nzito na kuleta maudhui ya kulalamikia mapenzi kwenye nyimbo zake.Lights....camera......action.... Ommy Kessy for you! P.U: KWA WALE WASIOKUJUA JINA LAKO HALISI NI NANI? A:Majina kamili nafamika kama omar Abdallah Jamali. P.U:ULIJITOSA KWENYE ULINGO WA MUZIKI LINI? A:Nilianza mziki nikiwa darasa la saba ilikua mwaka wa 2003 ila nilikua sina uwezo wakuingia ila nilijibambanya mwaka wa 2008 nilijuiunga na mwamba recods. P.U: BAADA YA KUJIUNGA NA MWAMBA RECORDS KWA NOOR MWAMBA LIPI LILIFUATA? A: Hapo ndipo nilipopata mafanikio baada ya hapo nilijiunga na Rage music hapo ndipo jina lingu lilizidi kuvuma kwa vibao motomoto. P.U: TUAMBIE BAADHI YA NYIMBO ZAKO ZILIZOVUMA A: Silali,Jeraha na kibao nilichokiwachilia juzi kwa jina nitulize.