Posts

Showing posts from July, 2017

YAKWETU BAND : ISINGEKUWA LIZZ JASOLJAH BASI TUSINGELIJULIKANA!

Image
Band inayopeta kwa sana tu, Yakwetu Band imetoboa siri ya mafanikio yao. Kikundi hiki kilichoanza anza mbwembwe zake mwaka uliopita 2016 kimemtaja Lizz Jasoljah kama msingi wao wa kutoka kimuziki. "Kusema ukweli ule, isingelikua Lizz basi tusingefika tulipofika. Manake tulipojuana naye ndio mambo yetu yalianza kufunguka na yuyu huyu Lizz ndiye aliyetupeleka kwa producer Ammz na tukarekodi ngoma kwa jina Olele. "Walieleza vijana hao. Yakwetu, ilipata umaarufu wa haraka jambo lililopelekea wao kuchaguliwa kama nominees wa Pwani Celebrity Awards. Kwa sasa ngoma yao ya ''sugar" ipo hewani na inafanya vyema Sana.

PRODUCER WA PWANI AFUNGUKA MENGI KUHUSU SANAA YA PWANI. SOMA ZAIDI HAPA!

Image
Produza msanii Lameck Boy wa Neptune records alifunguka mengi kuhusiana na sanaa ya Pwani hapo jana,25th. 7.2017. Lameck Boy aliongea haya baada ya kuona msukosuko flani ndani ya dau hili la muziki wa Pwani. Tukinukuu.... " Sanaa ya Pwani kikweli iko na muziki mzuri,ambao mtu anaweza penda kuusikiliza nakuushabikia,wasanii wako wenye bidii,maproducer wazuri pia,watangazaji pia wazuri wanaosapot muziki.Wako wasanii tajika kama Susumila,Ally B,Nyota Ndogo,Chikuzee,Sudi Boy,Dogo Richie,Fat S,Fisherman,Escobah,Simon Simz na wengine,wako maproducer tajika,nikiwemo,akiwa pia P Baindo,Amz,Emmy Dee,Toti,Noor Mwamba,Tk2,J Crack,Lai,P Lion,Mobiz na wengi ambao tunafanya kazi nzuri. 2;Vitu ambavyo vinaweza au vinarudisha nyuma sanaa ya Pwani ni vitu vitano.... " 1. Wasanii kutopendana,kutofanya kazi pamoja,wasanii kujiona bora kumliko mwengine. 2. Maprodusa pia kukosa kuja pamoja nakushirikiana,wengine kujiona wao ndio wakali kuliko wengine,produsa kujifanya anajua kila kitu,k...

RAPPER KNAMY KREEZY SHARES TEN THINGS YOU DIDN'T KNOW ABOUT HIM

Image
Fast uprising rapper Knamy Kreezy shares some secrets we didn't know about him. The Thika based trapstar was raised in the Coastal parts of Kenya and later shifted to Thika with his family. Read on.... Lights........ Camera...... Action!!!! Here is Knamy Kreezy for you!!! 1) I can do any type of music but people think I only do hiphop. (This is true) 2) I dont have a sports club(specifically football) although I really love sports. (Okay....) 3)The girl I'm dating right now is the first that am being faithful at. (that means he's been a player to all the other chicks.....mmmmmhhh) 4) Ive always thought of doing gospel music in my life but found myself doing secular. (Thats the voice of God calling, don't ignore it, hell fire is waiting!) 5)I got my first tattoo when I was 13 years old.   (OmG!!! Tatto at 13? Most of us would have been disowned by our parents) 6) I cannot sit down and listen to my first song and I dont even have it in phone be...

RAPPER OHMZ LAW MOMBASA AZINDULIWA KWENYE DOCUMENTARY YA HIPHOP SAVES LIVES

Image
Rapper gwiji ambaye vilevile ni mshairi mkali, Ohmz Law Montana ameshirikishwa kwenye documentary ya kimataifa kwa jina Hiphop Saves Lives. Ohms, amekuwa mstari wa mbele katika harakati za kuenua jamii kupitia hiphop. Jamaa huyu vilevile ameandaa video kali chini Ya director Johnson Kyalo.

MIMI SI PETER MSECHU WALA SIHUSIANI NAYE.MSANII WA TAVETA AONGEA.

Image
MIMI SI PETER MSECHU WALA SIHUSIANI NAYE.MSANII WA TAVETA AONGEA. Msanii anayeibukia kwa kasi sana, Nashipai ameamua kuongea kuhusiana na swala lake la kuitwa Peter Msechu. Nashipai, anayetokea Taita Taveta aliyaongea haya baada ya video yake ANGEJUA aliyomshirikisha msanii wa Bongo linex kutoka. "Watu wengi wanasema video ile ni ya Msechu na Linex ndiye aliyepiga kolabo Na Msechu ilhali ni mimi. Kweli twafanana kimpango ila sihusiani naye wala ile nyimbo sio yake. Nyimbo ni yangu nimemshirikisha Linex. "Alitueleza kupitia njia ya Simu. Tazama hapa video yenyewe iliyoandaliwa Na X Benjoes....... https://youtu.be/yO6GAjwdqLc

SABABU KUU YA KIGOTO KUKIMYA KUFICHUKA!!!! SOMA HAPA!!!

Image
SABABU KUU YA KIGOTO KUKIMYA KUFICHUKA!!!! SOMA HAPA!!! Aliwika sana na kujizolea sifa kem kem kutoka kwa mashabiki sio wa Pwani bali Kenya nzima. Tunamzungumzia msanii sifika Kigoto Mbonde. Staa huyu wa Kichapo cha Mapenzi alitoa hit kali kali zilizomfanya kuwa kipenzi cha watu. Kigoto alifanya kazi studio kadhaa ila urafiki wake wa karibu sana ulikuwa kwa studio ya Produza Tk2,hapa tunazungumzia Hornet Records Na baadae Number one records. Baada ya purukushani zisizoeleweka Kigoto alikatiza muziki ghafla na kunyamaza zii. Majuzi alirudi kupiga collabo Na Mswazi Masauti ambaye amenyamaza vilevile, nyimbo ikijulikana kama "Sawa." Cha kushangaza nyimbo hii haikupokelewa vyema Na ikabidi Kigoto kuingia mitini. Meza yetu ya habari ilichukua jukumu la kuwasiliana na Kigoto kuhusiana na ukimya wake na hapo ndipo tulipobaini kuwa jamaa huyu alikua masomoni. "Wajua mimi nilipomaliza shule ya upili, moja kwa moja nikaanza muziki hivyo sikupata nafasi ya kusoma. Sasa ku...

RINGA TALEMO AWACHIA VIDEO MPYA AKIWAHIMIZA WASANII WAFANYE VIDEO ZAO NA WAAANDALIZI WA PWANI

Image
Msanii Ringa Talemo Leo hii ameachia video yake ya Nipe Nipagawe chini Ya uandalizi wake produza Nau. Talemo alirekodi wimbo wake ndani ya Thundersounds kwa produza Morbiz almaarufu Sherrif na akaamua kufanya video papa hapa Pwani. "Nilionelea kazi hii nishughulikie hapa kwetu Pwani kwani waandalizi wa video wamekua wengi na wanajaribu sana kwa kazi zao.Kama wana uwezo kwanini tusikuzane sisi kwa sisi. Haina haja twende hadi Nairobi kufanya video ilhali Pwani kunao walio Na uwezo kama vile Produza Nau aliyedirect video yangu ya Nipe Nipagawe. " Alieleza Ringa Talemo kupitia njia ya simu. Tazama video hapa Na uone kama imeweza ama bado ------ >>> https://youtu.be/xGY5ALg0T8A

SHINEY ANNE ARUDI TENA KWA WIMBO WA AMANI

Image
Huku Pwani ikizidi kudorora kwa wasanii wa kike, msanii Shiney ameamua kurudi kimuziki. Shiney Anne, aliyevuma kwa vibao vikali vikali kama ride on me, ilingi, kilio Na vinginevyo alizima ghafla na kupotea kwenye ukumbi wa sanaa. Tulijaribu kuwasiliana naye Na alikua Na haya ya kutueleza, "Sio kuwa nilikimya kwa ubaya ama kwa kushindwa na muziki ila majukumu kadha wa kadha niliyafuatilia na pia nilitaka kuchukua break ili niweze kusoma huu muziki vizuri zaidi. Hata shule pia huwa kuna vipindi vya mapumziko. Hivyo basi mimi pia nilikua kwenye kipindi cha mapumziko na kwa sasa nipo tayari asilimia moja kuwapa burudani, kuhamasisha jamii na kuwa kielelezo chema kupitia muziki. " Shiney kwa sasa yupo matayarishoni ya kuachia kibao kipya kuhusu amani. Wimbo huo umetayarishwa na produza Baindo chini Ya Bigfoot production Na utawachiliwa rasmi tarehe moja mwezi wa Agosti.

PIGA KURA KWA REDIO SHOW BORA ZAIDI KUONA PWANI HAPA!!!!!

Image
Pwani Usanii Blogspot inafanya Survey ama upelelezi wa redio show kali zaidi mkoani Pwani. Je wewe hupendezwa Na show gani kati ya hizi : --->>> A. KAYA FLAVAZ YA RADIO KAYA B. MWAKE MWAKE YA PILIPILI FM C. MMU(MASHAV MASHAV) YA PWANI FM D. MZIKI MZUKA YA BARAKA FM BONYEZA HAPA>>>>>>>UPIGE KURA------ >>>>> https://strawpoll.com/wd848yad#.WW-YUuLanaU.facebook - - - - - - - - - - >>>>>>>KISHA WAWEZA TOA COMMENT YAKO. MWAMBIE MWENZIO PIA!!!!!!!!

NITAWALIPISHA WASANII WA PWANI WAKITAKA COLLABO - MSANII ASEMA

Image
Rapper anayetokea magharibi mwa Kenya, Noble Mirror amekua mwingi wa ghadhabu Na kutoa maneno ambayo tunaweza sema ni kama kejeli. Noble Mirror anayejiita Mwamba wa Magharibi alisema kuwa wasanii wa Pwani pamoja Na maproduza hawajui lolote Na wakati umefika waambiwe ukweli. "Kati ya wasanii ambao hawajui wanachokifanya ndani ya tasnia hii ya mziki ni wasanii kutokea mombasa na baadhi ya producers wao. Mfano , Mimi nikiwa katika tour zangu Coast nimewai kutana na wasanii na producers kadhaa wakaniomba collabo nikakubali kiundugu na pia tukapiga kazi Kali tu. Kati ya kazi nilizopiga nao niliwasihi nizipeleke Nairobi kwa producers wazuri zaidi kisha zifanyiwe mixing nzuri ila wote waliishia kukataa na mwishowe kupiga mixing mbovu. Hii inafanya niwatolee macho wasanii wa coast kali na kuwalipisha collabo ndio mwisho wa siku awe na bidii ya kuingiza kazi kwa soko. Kuhusu producers nitakuwa mkali sana kwa yeyote anayefanya kazi ya sauti yangu ju najielewa Sana na pia nina sau...

HAKUNA KUNDI LA KUTUTISHA - YAKWETU BAND YAAMKA!

Image
Band ya muziki ya Yakwetu imeamua kuleta vurugu kwenye ukumbi wa sanaa. Band hii iliyotambulishwa na produza Ammz baada ya kutoa kibao chao Olele na kuingia mitini imerudi kwa kishindo kwa kazi mpya kabisa. Baada ya kuwasiliana na kundi hili, Yakwetu walitueleza kuwa kwa Mara ya kwanza walikua wamekuja kutazama tu Sanaa Na kufanya upelelezi kuhusu muziki wa Pwani Na wa Kenya kwa jumla. "Tulikua tumeambiwa kwamba muziki hasa hapa Pwani ni mgumu mno kwa hivyo tukaamua kuyajaribu maji ya sanaa tupime kimo chake Na tulipogundua kwamba tunao uwezo basi sasa ndio kazi imeanza rasmi. Tulidhani Kuna wakali kutuliko sisi ila hataa..... Pwani hakuna wa kututisha na wimbo wetu mpya Sugar lazima utaingiza hela Nakutuvusha hadi ng'ambo ya Afrika mashariki. "Alieleza mmoja wao. Wimbo wao Sugar umeandaliwa Na produza Ammz ndani ya Tempoz records Na hivi karibuni mtauskia. Yakwetu ni ya Kwetu kweli!!!!!!

RAPPER RAPKEED AVUNJA UKIMYA.

Image
Rapper anayetokea kusini mwa Pwani, Diani, amevunja ukimya wa muda mrefu sana. Hii ni baada ya yeye kuandika Na kudokeza kuwa anawachia wimbo mpya. Msanii huyu aliyesikika kwa Mara ya kwanza kwa kibao chake 'dear mama' alitoa mfululizo wa nyimbo kadhaa ndani ya studio za Bigfoot music Na kukaa kimya zaidi ya Mwaka mmoja. Rapkeed kupitia Facebook alidokeza kuwa yupo na ujio mpya kwa jina SLOW DOWN uliofanyiwa makamuzi na produza Baindo. Tusubiri tuone mapya haya ya Rapkeed.

MSANII?????? HIVI BEKA THE BOY ANAMCHIMBA NANI KWENYE WIMBO HUU????

Image
MSANII?????? HIVI BEKA THE BOY ANAMCHIMBA NANI KWENYE WIMBO HUU???? Guu mosi guu pili ndivyo walivyonena wahenga, na hapa guu hili lazidi tembea kilomita nyingi hatua baada ya nyingine. Misemo kando, baada ya msanii kutoka chocolate city Malindi kuachia vibao motomoto kama Niko low, Siri ya Moyo (akimshirikisha Kiwanja) Na Maneno. Beka amerudi tena Na raundi hii amekuja kwa vijembe. Vijembe???? Jiulize tena, Beka ametayarishiwa kibao Na produza Ammz kinachoenda kwa jina Msanii. Swali ni je wimbo huu wamchimba nani? Je Beka katoa malalamishi yake ya changamoto za muziki? Au je msanii huyu amemdiss msanii fulani? Majibu utayapata dakika yoyote wimbo ukitoka...... Usikae mbali

AKOTHEE MTETEZI WA HAKI ZA KINA MAMA WALIOACHWA: VIDEO MPYA baby daddy

Image
Kwa jina anajulikana kama Akothee ukipenda waweza muita Madam Boss. Mwanadada huyu anayevuma kila mahali kwa ukwasi wake na muziki wake wa hali ya Juu ameamua kutoangalia nyuma. Akothee, ameachia video inayoangazia mateso apitiayo mama anapowachwa Na mume. Huku visa vya dhuluma za wanawake zikizidi kwenye jamii, Akothee ameamua kuwa kielelezo Na mtetezi wa wanawake kwa kueleza mateso, utengano Na chuki anazolimbilikiziwa mzazi wa kike. Video yenyewe imefanywa Na Hamza Omar wa One Montage films. Itazame hapa - - - - > https://youtu.be/NVRTNO8TPsA

ONE ON ONE NA MADINI CLASSIC:VITU VITANO USIVYOVIJUA KUHUSU!!!!

Image
Leo tunawaletea msanii Madini Classic aliyejulikana kitambo kama Philowize Madini.  Maneno haya bila kuongeza lolote yametoka kwa Madini Classic moja kwa moja.....   VITU VITANO WATU HAWAJUI KUKUHUSU..... TUELEZE 1.A lot of people think am not Akenyan I am aKenyan Born and raised in Nyanza.  2.People think 'Kwetu' cover is the song that paved my music ways while Uzuri Wako ndio wimbo uloinspire boss wangu anayenisimamia kwa saizi na ikamfanya kazi zangu zaidi.  3.Nimewahi Kutongoza Mwanamke mmoja tu in my life japo nimedate wanawake wengine pia lakini kwa Kutongoza nimewahi tongoza mmoja tu tangia kuzaliwa kwangu.  4.I strictly listen to East African music though I love international rappers but I don't listen to them as much as I listen to East African Music.  5.Sijawahi kuogopa wasafi kuiona kama kitu kubwa Sana'a hua naichukulia kikawaida yani kama wanamuziki wengine wanaofanya poa.  TAZAMA VIDEO YAKE HAPA---BONYEZA https://youtu.be/1uF0zrPazGo

HIPHOP TWAPAMBANA NAYO VIVYO HIVYO NA TUNATOBOA- RAPPER CHIDO D KINGA AFUNGUKA.

Image
HIPHOP TWAPAMBANA NAYO VIVYO HIVYO NA TUNATOBOA- RAPPER CHIDO D KINGA AFUNGUKA. Rapper anayetokea Kilifi Chibo D Kinga amefunguka na kutoa hoja zake kuhusiana na muziki wa hiphop Pwani. Msanii huyo alitetea sana muziki wa hiphop Pwani Na kusema kwa kasumba za kuwa hiphop hailipi zilipitwa Na wakati. Chibo,  aliongeza kuwa kila aina ya muziki kwenye karne hii ya Leo unalipa. Baada ya kumhoji zaidi jinsi au mbinu gani msanii hasa wa hapa Pwani anajilisha kupitia hiphop, majibu yake yalikua haya. "Msanii wa hiphop haifai ategemee radio na shows pekeake bali vpo vitu vingi yuaeza fanya na akajipatia pesa zake. " Vitu hivi vikiwa kama shows za kuhamasisha jamii kwenye shule, vyuo vikuu Na vya ufundi. Chibo-D Kinga alimalizia Na, hiphop sio ya kustarehe bali kufungua akili.

MANENO HAYA SIO SAWA.... MSANII AHIMIZA!!!!

Image
Sijui ni tetesi au tu maoni ya msanii huyu, Beka the Boy ambaye kwa sasa ndiye anayepeperusha bendera ya Pwani Juu zaidi. Saa zingine hali huwa sio hali kwenye uhusiano Na hapa Beka amejaribu kupitisha ujumbe wa Moyo wake. Swali ni je, msanii huyu yupo katika matatizo ya mahaba? Je Beka the Boy katemwa. Pata kujua ukweli wote kwa kuyatazama maneno aliyoyatoa kwenye nyimbo yake. Video hii hapa, tafakari...... BONYEZA LINK - - - - - - - - - >> https://youtu.be/slthFeHIzn0