Posts

Showing posts from May, 2016

MWANDISHI WA SANAA MANUEL NA RAPPER HUSTLA JAY WAZURU SHULE NA KUWAPA MOTISHA WANAFUNZI

Image
Mwandishi mashuhuri wa gazeti na maswala ya burudani Manuel Ntoyai na mwanahiphop Hustla Jay,walitembelea shule ya msingi ya TIMBWANI Baptist iliyopo maeneo ya Likoni. Wawili hao walitembelea shule hiyo kama moja ya miradi ya AFRICA IS NOW FOUNDATION kuwahamasisha wanafunzi kuhusu maswala ya jamii,elimu na taaluma,talanta na maswala ya madawa ya kulevya. Manuel ambaye ni kati ya wahariri wakuu na mwandishi wa sanaa na burudani wa gazeti la PEOPLE DAILY,majatida ya Spice na Tribe43 alikuja bayana na kueleza umuhimu wa utandawazi,elimu na taaluma naye Paul Maasai almaarufu Hustla Jay alizungumzia talanta na madawa ya kulevya mashuleni. Wawili hao Vilevile,tulipiwasiliana nao walisema huu ndio mwanzo tu ila watazuru shule na kuhamasisha wanafunzi zaidi ili kuwasaidia kwenye safari yao masomoni.
Image

HARUSI YA AKOTHEE YANUKIA NA JE MWANADADA HUYU NI MJA MZITO????pata majibu hapa!!!

Image
Nyota Ndogo keshatwaliwa,anayefuatia kwa laini ni Akothee.Mwanadada huyu mwenye vibao motomoto kama 'give it to me' na 'Mama-Shangerera' meza yetu ya habari imevumbua uvumbuzi kuwa harusi yake na mpenziwe wa Switzerland huenda ikiwa tarehe tano mwezi wa November. Vilevile Akothee alibandika picha na maandishi yanayozua maswali mengi sana. Maneno yenyewe yaligusia mambo na uja uzito na kama tunavyokumbuka tayari mwanamuziki huyu ni mama mlezi wa watoto watano....wasita yupo karibu. Akothee aliandika hivi......."While you are still in my past am already enjoying my present, baby no. - loading am blessed Akoth .this concoction is only ment for pregnant people it's full of iron & positive energy you know, but don't try this at home get the formula from me #madamboss" Kwa sasa Akothee yupo holiday Ulaya akasherekea siku yake ya kuzaliwa. HABARI NDIO HIYO.....HATUNA CHA KUONGEZA!!!!

WATANGAZAJI WA RADIO WALIONA MISHAHARA MINONO !!!!

Image
5.MUNENE NYAGAH WA Q FM. Kiwango chake kinaenda hadi 300,000 ksh. 4.KALEKYE MUMO WA KISS 100 FM Huyu binti ambaye vilevile ni msanii,ana kula hela urefu wa 300,000 ksh. 3.MBUSI WA RADIO JAMBO. Jamaa huyu aliyetoka mitaani na kujiunga na redio kwa neema ya Mungu anasheherekea zaidi ya nusu milioni kila mwezi. 2.CHURCHILL WA CLASSIC 105. Ucheshi wake ndio unaopamba kipindi chake pamoja na Maina Kageni kila kukicha.Milioni moja pesa za Kenya ndio zake kila mwisho wa mwezi. 1.MAINA KAGENI WA CLASSIC 105 Nambari ya kwanza ni ya huyu jamaa ambaye kila mwisho wa mwezi akaunti yake ya benki inaingia 1.5 M.

NYOTA NDOGO AZAWADIWA GARI KAMA ZAWADI YA HARUSI(Cheki photo hapa)

Image
Mama mlezi wa pwani yaonekana ashapata wa kumtunza na kumtunuku asilimia moja moja. Nyota Ndogo amezawadiwa gari kama Zawadi ya harusi yao.

NYOTA NDOGO AFUNGA HARUSI(picha zipo)

Image
Mlezi wa sanaa ya pwani,Nyota Ndogo hapo Jana alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa kizungu. Harusi hiyo iliyofanyika hapo Jana mjini Voi ilikuwa na sheshe kibao japo baadhi ya jamaa na familia kutohudhuria. Nyota amefunga harusi na mpenziwe mwenye asili ya kijerumani na harusi yenyewe itachukua siku mbili. Harusi ya Jana ilikuwa ya kidini na watu wa familia pekee na ya siku ya Leo (22,May,2016) ni ya kila mtu. Habari zinazotufikia ni kuwa ng'ombe kadha wamechinjwa kwa ajili ya sherehe hiyo na wageni pamoja na mashabiki zake Nyota Ndogo wamejaa furifuri kushuhudia na kusherehekea tukio lote.

BARUA KWA WATU WA UKUNDA!!!!!

Image
BARUA YA UKUNDA(UK)/DIANI BEACH KUTOKA KWA DADDY Q. Leo nimekesha studio nikifanya kazi huku nikiskiza kazi za nilipotoka Ukunda city south coast kwale county aisee siogopi kusema ukunda believed n made me,nilianza Grip wear ukunda,i got my first daughters in ukunda,i got my wife in UK and im proud of that,ukunda ni town utajua ki german kwa streets kuna watu washa save wakaruka mpaka ng,ambo lakini sasa ni machizi wamesota kama kitambo,i had a dream though i came from the ghetto i,m the first rapper to put ukunda on the map musically with back to back hits enzi Brown mauzo alikua boy wa kunipelekea bling kuoshwa kwa sonara,enzi George Uduny aka Kingstin ni maniac mighty pigo,enzi Rudi Wu Makeke bado yuko makeke family na kina cliff hajashika bazooka la kenya army,enzi Producernau Mzee Wakilingile na Produza Noor Mwamba bado ni wasanii,enzi Fisher Man na Sharo Baro Sketcher hawajaanza kuvaa zile belti kubwa zimepigwa welding,enzi Tk Mbili hajajua kutumia fruity loops,enzi hatukujua M...

HARUSI YA NYOTA NDOGO KWA MPENZI WAKE WA KIZUNGU YALETA MGONGANO WA KIFAMILIA.

Image
Baada ya kupata mpenzi wa kizungu na kuonyesha mahaba motomoto hadharani,msanii Nyota Ndogo ameamua kupeleka mahaba level zingine. Jambo hili laonekana kutoenda vyema na nduguye kwa jina Juma Tutu anayeimba Swahili Jazz.Juma aligadhabishwa na Nyota kwa kupanga na kuandaa harusi ambapo tuliyoyasikia ni kuwa mahari haitalipwa kwa familia ya Nyota Ndogo. Hatuandiki mengi,jisomee snapshots zenyewe hapa!!!!!

DULLY MELODY AONYESHA TATTOO YA MENEJA WA DAZLAH;LIZZ JAHSOLJAH!!!(picha zipo!!!!!)

Image
Baada ya msanii anayechipuka kwa kasi Dully Melody kuchora tattoo ya Lizz Jahsolja ambaye meneja wa Dazlah,tetesi zilizuka eti ilikua uongo. Dully alidinda kuonyesha mchoro wake wa tattoo na jambo hili lilimfanya kuwa kicheko cha watu na mashabiki zake pia. Kumbe siri ilikua kwa YAGAYAGA nyimbo yake mpya. "Hii tattoo ilikuwa ni kama Zawadi kwa Lizz kwa hiyo nilingojea wakati mwafaka wa kuionyesha hadharani na wakati wenyewe ni huu ambapo nyimbo yangu YAGAYAGA ipo tayari." Alieleza Dully.Pata kuidownload nyimbo yenyewe hapa ------------- >>>>> http://mdundo.com/song/54380

MUSICIAN GILAD FOR KENYAN CITIZENSHIP??? get the full details here!!!

Image
Gilad Millo, Kenya’s musician deemed as the ‘King wa mapenzi’ by his fans, has been quoted on several occasions speaking on his love for the Kenyan state. Outpouring his love first through his social media pages, and secondly in his music created for the Kenyan people by singing in a language that is close to them, Kiswahili. Gilad has attracted the name brother by many of the people who have come to meet him. Anyone who has met Gilad will tell you that he is humble, jovial, a real lifeist, a man of the people among other traits. Circulating around the internet is Gilad’s immigration application for Kenya Citizenship that he has presented to the Kenyan immigration office. This news has circulated to reach the news desk of renowned Journalist, Larry Madowo who asked the question on his leading show, the trend. This prompted a massive feedback from Kenyans pouring their heart out to welcome the decision with both arms with the hashtag #MakeGiladKenyan trending the whole of Friday 20t...

MSANII WA PWANI AINGIA BONGO NA KUPIGA BONGE LA COLLABO NA MZEE YUSUF MWENYEWE!!!!!

Image
Wengi wanamfahamu kama Single Jay,msanii anayetokea kusini mwa pwani. Single-Jay au ukipenda Jizze ni msanii anayefanya muziki wa hiphop na afrofusion.Jay alisikika kwa mara ya kwanza kwa wimbo MAMA uliofanya vizuri Japo sio sana. Mshikaji huyu alisafiri bongo kufanya collabo na wasanii wa huko waliomuita kufanya kazi naye. Kufika bongo wasanii aliokuwa afanye kazi nao walikuwa bize kidogo kwa hio Single Jay ikabidi aingie studio ya C9 na kufanya muziki peke yake. Jay alieleza hivi... "Washikaji wenyewe wa bongo wanajiita Kaka chotara,Steve Ghostwritter, Superboy na Kissy music.Hao ndio washikaji tulio organise hio kollabo na kusudi ya kollabo nikusambaza mziki wangu sio Kenya pekee tu bali Afrika Mashariki." PWANI USANII: HIVI JE ILITOKEAJE UKAPIGA COLLABO NA MZEE YUSUF??? SINGLE JAY:Wasanii hao wa Bongo walitaka niende tufanye ngoma ila bahati mbaya nilipofika wakawa wengine wameshikika kiasi sasa ikabidi tuondoe hio issue ila nikaona nikirudi bila kufanya ngoma ni...

Namba moja????CASH ERA AMTUMIA PRODUZA FLANI UJUMBE WA KEJELI!!!!

Image
Baada ya kumpasha Produza flani (tutakayembana jina kwa sasa ila siku yake itafika) kwa kusema Deborah ndio wimbo mkali pekee kwenye studio ya Produza huyo.Cash Era amerudi na vigoa vikali na kugoa studio flani. Msanii huyu aliyeachia kibao chake kwa jina CHIJEGO hapo juzi alimshukuru sana Produza Ammz kwa kumuokoa kutoka mikononi mwa "Wamisri"..... (hahaha).Vilevile aliongezea eti....kama ni Number basi Tempoz ndio moja!!!!! Haya jijazie!!!!

Pwani Usanii

Image
Hello there family and great friends. We need your help.Nominate this blog to be one of the blogs of the year in the forthcoming MOMBASA AWARDS. Send a text message PWANI USANII BLOGGER OF THE YEAR to 0706 187502. Thank you.

MWAMKO MPYA WA TUZO PWANI!!! ZENYE MIBABE YA WADHAMINI!!!

Image
Ni habari njema kwa tasnia ya sanaa ya pwani kwani mazuri tele yametufikia. Tunazizungumzia tuzo za MOMBASA AWARDS 2016 ambazo ndizo gumzo mitaani kwa sasa. Tulipowasiliana na mmoja wa waandalizi wa tuzo hizi alituarifu kuwa tayari mikakati kabambe ishawekwa na wadhamini kupatikana tayari. Wadhamini hao wakiwemo kampuni ya Coca Cola, kampuni ya simu ya X-tigi na wengi Kwa sasa mashabiki wanapaswa kutuma ombi lao la nominees wanaowataka kwa mombasaawards2016@yahoo.com. Vitengo ni kibao.......chaguo ni lako.....Hata hivyo msisahau kutuma pwani usanii kwa kitengo cha blogger of the year!!!!