KAA LA MOTO ANYOOSHA MKONO KUSAIDIA JAMII YA SPRINGS OF HOPE CENTER.
Kuimba tu na kuburudisha
hakutoshi ndio usemi mpya wa sanaa ya pwani.Huku Fisherman akimaliza
kuwakaribisha wenzake kwa 'TWAAYF KIDS BACK TO SKUL DONATIONS' rapper
Kaa la Moto amenakili kwenye ukurasa wake wa Facebook mambo mema
aliyokuwa akiwafanyia watoto wa mitaani na wasiojiweza wa Springs Of
Hope Watamu.Rapper Kaa La Moto alikuwa na mradi wa HAKUNA CHOKORAA,NI
BINADAMU PIA.Tukimnukuu kwenye kurasa zake za facebook Kaa La Moto
aliandika haya "As an mcee we do many projects mbali na mziki ...Inafika
muda una nyosha mkono kwa Jamii....Msanii ni kioo cha jamii sio kioo
cha Jaguar...Asante Mama Nyota Ndogo Kwa yote na harakati
tunazofanya...Nikiwa WATAMU the whole week with Street kids at Springs
of Hope....Big up kwa the Commitee am wit....Asante Mungu...Project
Hakuna Chokoraa ni Binadamu pia ...." Vilevile kutakuwa na mradi wa
TWAAYF KIDS BACK TO SKUL DONATIONS jumapili hii tarehe nne kuanzia saa
sita Likoni.Nyote mwakaribishwa kusaidia kutoa chochote
kitakachowawezesha watoto warudi shule kwa muhula wa pili.
Comments
Post a Comment