PRODUZA MSANII LAI AFUNGUKA VIKALI KUHUSU SUDI MANJEWA.



Huku akiwa tayari kuachia wimbo wake mpya,produza msanii Lai anayetokea pande za Kilifi na aliyevuma kwa vibao vikali vikali kama nipe risiti,kimya lai anaongea,lawama lazima na vinginevyo amekuja wazi na kuvunja ukimya wake na kuongea kuhusu tetesi zake na msanii Sudi Manjewa.Tulipowasiliana naye Lai alitueleza hivi....."Sina mpango wa kufanya collabo na sudi manjewa kama wengi wanavyodai,wala sikumtetea sudi nilipokuwa kwa interview na dj Gates,.yes,kuna story na mimi mwenyewe nishawai ulizwa kama ni kweli kuna ngoma yenye nimefanya na sudi manjewa ila tu tumeizuia bado,jibu ni NO,hakuna chochote na sijapanga lolote juu ya project naye,.yes i know Sudi ni msanii mzuri ila hayuko kwenye mpango wangu kwa sasa...." Lai tayari ashakuja wazi kuwa hana mpango wowote wa kufanya collabo na Sudi Manjewa na hajawahi fanya muziki naye.Lai vilevile aliongezea haya......."kuhusu kumtetea alipokuwa akikashifiwa na dj gates juu ya utunzi wake wa kudiss,mimi sikumtetea ila nilisema kulingana na ninavyomjua na kuujua mziki wake,nafikiri niliweka wazi kuwa..kama sudi amefanya ngoma na akaona mafans wameipokea vyema basi asibadilishe ila aendelee kuwapa wanachotaka na ikibidi aongeze bidii,na pia nawatahadharisha wasanii dhidi ya kujishuku pale tu mtu atoapo wimbo unaolenga jamii flani,kama ni wewe ni wewe na ni bora urekebishe ila pia hatuwezi kuwa sote,sasa tuache kujishuku bila mpangilio..kwa sasa ndio natarajia wiki ijayo kutoa nyimbo mpya ya style ya mduara kwa ajili ya mashabiki wanaopenda style hizo"

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA