KUTANA NA POLISI MSANII: KALLY D
TUAMBIE JINA LAKO RASMI NA LA USANII:
Kalume Dzombo aka Kally D.
UNATOKEA PANDE GANI YA PWANI?
Natokea Kilifi county.
UNA NYIMBO NGAPI KWA SASA?
Nimetoa ngoma tatu kwa sasa...Unaniweza..Hii Ngoma...Come baby Come...kwa sasa kibao changu kipya kinachoitwa CHEZA kimekubalika sana hasa Nairobi na kuchezwa kwa radio kadhaa humu nchini...ki bao hiki pia kimenipa umaarufu sana.
TUELEZE ZAIDI.
Yeah kibao Cheza kimeniwezesha kufanya interviews tatu kwa kipindi cha mwezi mmoja tu.
KANDO NA MUZIKI WAJISHUGHULISHA NA NINI?
Kally D ambaye pia ni Askari wa AP(Administration Police) najivunia sana kipaji changu maana kimenipeleka mbali sana.
LABDA UNA UJIO MPYA WOWOTE?
Yeah niko na wimbo ambao nimetayarisha mpya kwa sasa ambao natamani sana kuufanya na producer TK 2.
Comments
Post a Comment