SHEMBWANA MASAUTI ALIA MACHOZI BAADA YA KUSHUSHIWA MATUSI NA PRESENTA WA REDIO:
"Uko mbali nakutafuta,tamaa yangu haijakatika beybie we ndio unanifaa niko ritho usiku kucha.....!" Hio ndio chorus ya wimbo uliomtoa msanii Shembwana na wengi wakamhafamu.Wimbo 'uko mbali' ulifuatiwa na 'siwezi' ukampandisha kwenye ulingo wa sanaa ya pwani zaidi.Msanii huyu kwa sasa yuasononeka baada ya kupigiwa simu na presenta wa redio na kutukanwa matusi ya hali ya juu. Masauti hakujua kiini cha presenta huyo kumtusi. Kwa uchungu huku akibubujikwa kwa machozi,Shembwana alifululiza haya kwa ukurasa wake wa facebook.."hamuezi amini najua lakini Mungu pekee ndo shahidi yangu....napokea simu new number. Namuuliza nani mwenzangu alichokisema walai kilinishangaza...aliniambia we masauti wacha ushoga na akanitukania mamangu mzazi....niliamua kusave ile namba nikaenda watsapp maybe nitapata halafu nicheki profile yake kama ni nani kama kweli nikampata ni mtu ninayemjua tena presenter anaye heshimika sitamtaja* kwakweli alinifanya nikalia mchana mzima....ananitusi bila sababu.Mungu ndo nimemuachia tu" .Shembwana vilevile alikuwa kwenye collabo ya wimbo 'jitambulishe remix' ya rapdem na anao ujio mpya ila swali ni je,PRESENTERS WANAPASWA KUJENGA AU KUBOMOA?
Comments
Post a Comment