KALICHA ADAI KUWA HANA MKE ILA ANA MTOTO WA MIAKA MIWILI!!!
Kalicha,gwiji wa muziki aliyejimwaya uwanjani kwa kibao chake 'muda unasonga' na kurudi kutupatia 'shoboka' aliyoipiga na Sudiboy amepuzilia mbali uvumi unaotamba kwa sana ati ana mke nyumbani.Msanii huyo alikuja bayana na kuyaweka wazi maneno haya.Hivi ndivyo alivyolonga...."Mwanzo mi sijaowa ila nina mtoto wa miaka miwili na nusu niliye zaa na mwanamke aitwaye Eunice haya eti nasikia scandal eti nimeoa nakataa." Vilevile Kalicha alitueleza kuwa ana ujio mpya kimuziki na hivi ndivyo alivyoongezea "pili kuna debe naachilia kuanzia hivi karibuni liitwalo 'gazeti la leo' produza Tash gifted records.'
Comments
Post a Comment