THE RETURN OF MAJID KULEKULE!!!
Alipokimya wengi walijiuliza ameenda wapi? Majibu yakawa tofauti tofauti kama kawacha muziki,mara mgonjwa,mara karogwa mara kakimbia pwani.Walidhani atakimya milele daima ila hawakujua kuwa mfalme wa Uswazi almaarufu Majid Kulekule atarudi kwa kishindo! Majid ambaye yupo chini ya Jungle Masterz aliyevuma kwa vibao vya kusimua kama Senoura,Serebuka na Hali alikuwa kwenye collabo ya Lypso dogodogo remix.Vilevile tulipowasiliana naye,Majid alituarifu kuwa yupo kwenye uandalizi wa mambo mapya yatakayowasisimua mashabiki wa muziki wa pwani.Majid alituarifu kuwa wengi walidhani kuwa atapotea ila bado yupo imara na raundi hii bila shaka watamkubali zaidi.
Comments
Post a Comment