SUSUMILA AMALIZA TOFAUTI ZAKE NA RADIO KAYA HUKU MWANDISHI WA HABARI AKIMUOMBA MSAMAHA
Bingwa wa 'ngoma itambae' na kwa sasa 'Hidaya' Susumila au ukipenda zaidi Jembe wa majembe amesafisha tofauti zake baina yake na kituo cha radio kaya. Mwanamuziki huyo aliletwa pamoja na watangazaji wa kituo hicho kupitia ushirikiano wa msanii Chikuzee na produza Tk2. Tulipowasiliana na mtangazaji na director wa kipindi cha kaya flavours na chipkizi za Kaya,Teddy Nyae Wa Tinga alikuwa na haya ya kunena....
" Susumila amemaliza tofauti zake na Radio Kaya hii ni baada ya mikutano kadhaa iliyohusisha chikuzee,TK2 kabla ya yeye kuzuru Radio Kaya siku ya ijumaa iliyopita...."
Huku hayo yakijiri mwandishi wetu shupavu wa sanaa ya pwani, Godwin Wambua almaarufu Habari za Mombasani Usanii alimuomba msamaha msanii huyo baada ya kumnukuu na kuandika habari zilizoleta utatanishi ambao ulimchukiza Susumila.
Vilevile Susumila yupo na ujio mpya kabisa kwa jina 'Hidaya' aliomshirikisha Chikuzee.
Comments
Post a Comment