ROSE MUHANDO AZIDIWA NA MADAWA YA KULEVYA!!! KATOROKA NYUMBANI!!!
MAMBO yanazidi kumwendea vibaya staa wa zamani wa injili Rose Muhando ambaye sasa anaripotiwa kusakwa na kituo maarufu cha ushauri nasaha jijini Dar, Sober House.
 
Taarifa zinadai kuwa mwimbaji huyo anasakwa na uongozi wa kituo hicho ili waweze kumwokoa baada ya kutekwa na utumizi ya dawa za kulevya.
Chanzo kilicho karibu na mwanamama huyo kimeeleza kuwa ametoweka nyumbani kwake mjini Dodoma baada ya kulemewa na unga na sasa kiongozi mmoja wa dini anaripotiwa kujitolea kumsaidia.
“Kuna kiongozi mmoja wa dini hapa Dodoma amejitolea kumsaidia Rose baada ya kusikia hali yake ni mbaya zaidi.
Kaufuata uongozi wa Sober House wamsake popote alipo na wakimpata wampeleke katika kituo hicho moja kwa moja na gharama zote yeye atazishughulikia,” gazeti la Wikienda limearifu.
Comments
Post a Comment