ADILI TOZY AFANYA MAANDALIZI YA VIDEO YAKE.

ADILI TOZY AFANYA MAANDALIZI YA VIDEO YAKE.

Baada tu ya kujitambulisha kimuziki,msanii anayeibukia kwa kazi,Adili Tozy ameamua kuwaburudisha mashabiki kwa video ya wimbo wake 'Acha niseme'.

Nyimbo hiyo iliyotayarishwa na producer Lameck Boy inazungumzia swala linalokumba jamii na maudhui ya elimu na umaskini yamedhihirika vyema na kupewa kipao mbele.
"Niliona itakuwa jambo la busara iwapo nitawachia audio na kuwabamiza mashabiki zangu kwa video juu kwa juu.Japo bado nipo katika hali ya kukita mizizi pwani,sitalegeza kamba kamwe kwa sababu nimepata management inayonipa motisha na msukumo wa kufanya kazi pasipo shida yoyote." Alieleza Adili Tozy.

Video ya wimbo 'Acha niseme' uliandaliwa na kampuni ya Coastline photography and videos wikendi iliyopita na kampuni ya Remuked entertainment inayomsimamia msanii huyu imeahidi kuachia video hiyo kipindi cha wiki mbili zijazo.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA