EXCLUSIVE INTERVIEW: KWA MARA YA KWANZA KABISA KUTANA NA MSANII ADILI TOZY!
Pwani Usanii kama kawaida hupata fursa ya kuvitambulisha vipaji vipya na raundi hii tunawaletea msanii Adili Tozy aliye chini ya Remuked Entertainment. Soma zaidi.....
Pwani Usanii:Tuambie jina lako la serikali na jina lako la kisanii.
Adili Tozy:Jina langu la kitambulisho ninalotambulika nalo ni Ismail Chimwana Kahindi na la kikazi au nikipanda steji wananiita Adili Tozy.
Pwani Usanii:Swadakta kabisa. Je ulisomea wapi?
Adili Tozy:Nilisomea Kikambala primary school na kujiunga na sekondari ila Sikumaliza sekondari kwa sababu ya shida za kifamilia.
Pwani Usanii: Ni kitu gani kilichokufanya kuanza muziki?
Adili Tozy:Kitu kilichonifanya nianze muziki ni kuwa niliona wadogo zangu wakipaa na kufanikiwa kimuziki nami nikaamua kujitosa kwenye ulingo uo huo kwa sababu tayari kipaji nilikua nacho.
Pwani Usanii: Je wafanya muziki aina gani?
Adili Tozy: Nafanya muziki aina nyingi kwa sababu nina kipaji,naweza flow na mdundo wa aina yoyote. Ila kwa sasa napiga muziki wa malovey dovey,swahili rnb na afro-pop.
Pwani Usanii: Huu muziki uliuanza vipi kwa sababu tunavyojua tasnia ya muziki ina shida si haba na vilevile tueleza shida ulizokumbana nazo.
Adili Tozy:Nilianza muziki kishida,kama kufukuzwa studio na kudharauliwa nikiambiwa sina kipaji. Watu walikua hawajajua thamani yangu.Hawakutaka hata kunisikiza kamwe na pindi nikitaka kujieleza,maneno yangu waliyapuuza tu.
Ila vilevile Kuna baadhi ya watu walionitia moyo na kunipa msukumo kuwa naweza.Kwa hivyo sikukata tamaa kiurahisi.
Pwani Usanii: Umesajiliwa na kwa sasa unafanya kazi zako chini ya Remuked entertainment. Wajisikiaje kama msanii kupata fursa hiyo?
Adili Tozy:Kufanya kazi na Remuked entertainment ni kama zawadi kwangu kwa sababu imenipeleka mahali pazuri.Mafanikio yangu ni mafanikio ya Remuked na Mafanikio ya Remuked ni mafanikio yangu.
Pwani Usanii:Ungependa kufanya kazi na wasanii kina nani hapa pwani?
Adili Tozy: Kama ni Collabo basi ningependa kufanya na Chikuzee,Dazlah na Wasojali band.Hao napenda kazi zao na nina matumaini siku zijazo basi nitaingia booth moja nao.
Pwani Usanii: Tueleze kuhusu project zako za kimuziki kwa sasa.
Adili Tozy:Kwa sasa nimemaliza project yangu mpya yaitwa 'Acha niseme' ambayo ni true story kabisa iliyonitokea na nikaona niimbe ili nieleze kisa chote kupitia muziki.
Project inayokuja,inaitwa 'ningojee' na sio siri wala sio kwamba najisifu,kazi hizi mbili ni moto wa kuotea mbali. Natumai mashabiki watazipokea vyema.
Pwani Usanii: Kwa wasanii wanaochipuka,una lipi la kuwaambia?
Adili Tozy: Ningependa kuwapa motisha na kuwaambia kuwa kila kitu ni bidii na maombi,mafanikio yatakuja yenyewe.
Comments
Post a Comment