PATA KUMFAHAMU POUL IBRAHIM KWENYE ULINGO WA MODELING.
Pwani Usanii: Jina lako wajulikana kama nani?
Poul Ibrahim:Poul Ibrahim
PU: Tueleze kiasi kuhusu maisha yako ya utotoni.
Poul Ibrahim:Nilizaliwa Likoni,mitaa ya Kiwerera pale Karibu na flats. Nikasomea Likoni Muslim primary na kujiunga na Pwani secondary school.
Hapo ndipo nilianza kufanya uigizaji kwenye tamasha za drama na music.
PU:Vyema kabisa. Katika uigizaji labda ulipendezwa na nini?
Poul Ibrahim: Nilipendezwa sana na vile nilivyokua najieleza mbele ya umati na vilevile nilikua dancer mkali sana.
PU:Na labda ulianza lini mambo ya modeling?
Poul Ibrahim: Modeling nilianza high school ila sikua serious serious sana hadi nilipomaliza shule kwa sababu ya masomo.
Nilipomaliza masomo hapo ndipo nilipojimwaga uwanjani.
PU: Wewe kama model wa kiume umefanya mambo kama yapi?
Poul Ibrahim: Nimekua kwenye mashindano na tamasha tofauti za modeling na vilevile nishakua kwenye advertisements za kampuni moja-mbili hivi.
PU: Lengo lako kuu hasa ni nini?
Poul Ibrahim: Lengo langu kuu ni kuhasisha watu kuwa modeling kwa wavulana pia ipo na ukitia bidii unaweza fanikiwa.
PU: Shida gani unazopitia kama model wa kivulana?
Poul Ibrahim: Shida ninazopitia au tunazopitia kama models wa kiume ni kupata watu wanaothamini kazi yetu,kwa sababu watu wamezoea models wa kike pekee.
PU: Labda mtu akitaka kukufikia anaweza kupata vipi?
Poul Ibrahim: Anaweza kunipata kupitia Facebook Poul Ibrahim au kupitia nambari yangu 0704 40 69 97.
Comments
Post a Comment