KUTANA NA ZIKY WA ZIKY: MWANAWE EMMY DEE
Studio ya Justers masters inafahamika sana kwa ulezi wa wasanii wapya.Chini ya mbawa zake produza Emmy Dee na Malezi yake Prince Adio kutana na kipaji kipya kabisa,Ziky wa Ziky,,,,
Pwani Usanii:Tueleza Ziky ni nani?
Ziky:Mimi ni Ziky aka Ziky wa Ziky,mzaliwa wa Kwale.Kazini Ukunda Ibiza.
Pwani Usanii:Ulianza muziki lini?
Ziky:Nilianza mziki mwaka wa 2010 ila kurekodi ilichukua muda.Sikuwa na kazi wala familia ya kunisaidia.Ilichukua miaka mitatu kuurekodi wimbo wangu wa kwanza ambao n MAMA WANANGU,studio ya Jungle Masters kwa produza Emmy Dee.
Pwani Usanii:Changamoto zipi unapitia kama msanii?
Ziky:Kama tujuavyo kuitwa msanii ni kitu rahisi ila kulijenga jina liwe kioo cha jamii inachukua muda.
Pwani Usanii:waweza sema muziki umekufikisha wapi?
Ziky:Kwa sasa Emmy Dee ndio mzazi yaani yeye ndio anausimamia mziki wangu na namshukuru kwa kunipa nafasi hio nilokua nikiitamani kwa hamu kuu.
Pwani Usanii:Ziky waweza toa shukurani kwa nani na nani?
Ziky:Nawashukuru radio presenters,jungle crew na mashabiki wote kwa support mnayonipa.Niliwahitaji, Nawahitaji na nitazidi kuwahitaji,kwani bila nyinyi hakuna step nitapiga.Hata mbuyu ulianza kama.......
Pwani Usanii:...Ulianza kama mchicha! Unakubali wasanii kina nani hapa pwani?
Ziky:Wasanii ninaowakubali ni DOGO-RICHIE,MAJID,DAZLA KIDUCHE NA NYOTA-NDOGO. Napenda sana utunzi wao japo wapo wengine pia.
Comments
Post a Comment