SABABU KUU ZA KUFIFIA KWA SANAA YA PWANI: PROMOTER NOTTYSTEE AONGEA.

Sanaa ya pwani kila uchao yasemwa kuwa yadidimia ilhali vijana ni matajiri wa talanta tofauti tofauti. Katika pitapita zetu tulipata nafasi ya kumhoji Promoter Nottystee
gwiji hapa pwani na hivi kuhusu sanaa.Na alikuwa na haya ya kusema:

Pwani vipaji vipo kwa wingi ila kuna mambo kadhaa yanayovuta sanaa hii nyuma na kuididimiza sana.Jambo la kwanza kabisa ni poor management ya wasanii.Management ya usanii ni gharama na msanii awe wa kuimba,kuiga,kucheza,modelling au wa aina yoyote ile kama hatopata mfadhali atakaye msimamia kila kitu basi juhudi zake zitaambuli patupu.Sababu ya pili ni viongozi hawasupport usanii sana kama inavyotakiwa.Viongozi hawafuatilii wala hawaanzishi miradi itakayo wapa vijana nafasi ya kujiajiri kupitia sanaa.Jambo la tatu ni kuwa radio za pwani haziskiki Kenya nzima kwa hivyo wakati wanamuziki wa pwani wanapojibidiisha kufanya kazi zao na kuzipeleka kwenye vituo hazivuki mipaka ya pwani.Wanamuziki wanaishia papa hapa pwani.Hizi ni baadhi tu ya sababu kuu zinazoua sanaa ya pwani.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA