KUTANA NA MSANII WA KIZAZI KIPYA KEN-MWENYEWE AFISA WA KWS ANAYEPIGANIA HAKI ZA WANYAMA PORI.


Ni Afisa wa KWS ambaye anafanya muziki na amejitolea kufa kupona kulinda wanyama pori.Tulipata kumhoji Ken na hivi ndivyo mambo yalivyojiri.....
Pwani Usanii:Wanakuitaje jina lako halisi na lile la usanii?
Ken:Jina halisi la kitambulisho ni Kennedy Opiyo Onyango na la usanii ni Ken Mwenyewe.
PU:Una miaka mingapi?
Ken:Mi bado mtoto,nina 24 tu.
PU:Unatokea wapi?
Ken:Mi ni mzaliwa wa pwani na naishi Kinango ila nafanya kazi ya kulinda wanyama(KWS) Nairobi.
PU:Ulianza muziki lini?
Ken:Muziki nilianza nikiwa na miaka ishirini nikitunga rap music ila baada ya muda nikaona kipaji changu kina uzito sana pande ya rnb.So,naimba swahili rnb.
PU:Tueleze kuhusu wimbo wako wa kwanza.
Ken:Wimbo wangu wa kwanza nilirekodi Ziky records chini ya produza Johny Blaze.Wimbo wenyewe uliitwa saluti wa kuhamasisha jamii ili waweze kuona manufaa ya kuwalinda wanyama pori.
PU:Kazi nzuri.Kuna wimbo wako uliovuma kwa jina 'mama usinifiche'.Tueleze kuhusu wimbo huo.
Ken:Wimbo huo niliurekodi Real records studio iliyopo Nakuru chini ya produza UnderwaterVideo nayo ilandaliwa na Nezzoh wa Safi Entertainment.Wimbo 'mama usinifiche' ulizungumzia mambo ya kawaida yanayomkumba mtoto kwenye jamii.Kutojua babake mzazi halisi.
PU:Vyema.Mashabiki watarajie nini kutoka kwako hivi karibuni?
Ken:Kuna collabo nafanya hivi karibuni na Jalemla ambaye ni ofisa wa Kenya army.Wimbo wenyewe utakuwa wa kuhamasisha mambo ya amani nchini.
PU:Lengo lako kuu kwenye muziki ni lipi?
Ken:Lengo langu ni kuifunza jamii kupitia muziki hasa kwa mambo ya kutunza mazingira na kudumisha amani.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA