KUTANA NA PHILO BLIVER:MSANII PRESENTA
Pwani usanii:Ulianza muziki lini?
Philo Bliver: I joined music industry last year 2013 nilikua kwa group twajiita Believers family ya watu watatu ndugu zangu.
Pwani Usanii:Bado kundi hili lenu lipo ama?
Philo Bliver:Kwa sababu niko mbali nao mara nyingi mi huimba tu peke yangu.
Pwani Usanii:Una yapi ya kuwaambia mashabiki zako?
Philo Bliver:Nashukuru Mungu ju watu wengi waliosikia kazi zangu wanazidi kunipa moyo wa kusonga mbele zaidi.
Pwani usanii:Mbali na usanii,wajihusisha na nini?
Philo Bliver:Mbali na usanii mimi pia ni mwanahabari wa Sheki f.m reporter pia presenter.
Pwani Usanii:Lengo lako kubwa kwenye sanaa ya muziki ni ipi?
Philo Bliver:Lengo langu kubwa ni kutaka kuona kwamba watu wanasikia nyimbo zangu Afrika mashariki na ulimwengu mzima.
Pwani Usanii:Wewe kama presenta unaweza saidiaje wanamuziki wenzako?
Philo Bliver:Niko tayari kukuza vipaji ambavyo mpaka sasa vipo chini ya maji.Msanii yeyote anayefanya gospel yuaweza nipa nyimbo zake bila hata shilingi ili niziwe kuzicheza ndani ya 106.6 sheki f.m twavuma twaskika.
Pwani Usanii:Wapenda nini zaidi kwenye tasnia ya muziki?
Philo Bliver:Ninachopenda zaidi ni kuona vipawa vikifanyiwa kazi na watu wakiendelea mbali na kufuata ya watu eti huezi kutoka ukiwa mombasa mpaka uende Nairobi.Najua kila kitu chawezekana ukiwa na bidii pia umuweke Mungu mbele.
Comments
Post a Comment