KUTANA NA KING WA RHUMBA KENYA ANAYETOKEA PWANI: PRINCE CHEF DE ETAT MAJOR
Leo tumepata kumhoji mkali wa miondoko ya rhumba na lingala anayetokea papa hapa pwani ila amechukua cheo cha ufalme wa rhumba Kenya nzima.Jina lake ni Prince Chef De Etat Major.
Pwani Usanii: Prince Chef de Etat Major ni nani?
Prince Chef:Jina langu kamili naitwa Prince Odhiambo.Nilizaliwa mitaa ya Barsheba papa hapa Mombasa.
Nilikuwa mwana muziki na Banoko international du congo Mombasa miaka minne.
Pwani Usanii:Sasa tupe safari yako ya maisha kwenye ulingo wa muziki wa rhumba.
Prince Chef:Niliingia pwani fm kama assistant producer nikimsaidia dada Tima Kisasa kwa kipindi cha rhumba kila Jumamosi. Sikukaa sana nikaenda Nairobi pale nilingia Ktn nikawa nasaidiana na Mwashumbe wa radio maisha kuleta wanamuziki wa Congo pale kuhojiwa na kucheza miziki yao.
Kisha nikaingia pale kwa kipindi cha rasha rasha KTN pia kazi hio hio mpaka mwisho ndio nikajiunga na pwani tv october.
Pwani Usanii: Unajihusisha na nini kwa sasa?
Prince Chef: Kwa sasa niko na kipindi kiitwacho NGOMA KITOKO pwani tv kila jumamosi saa 4 na kila siku saa nne usiku.
Pwani Usanii:Una malengo yapi miaka ijayo kwenye sanaa ya rhumba?
Prince Chef:Vision yangu ni kufungua radio station yangu na ni kupromote wanamuziki wa kizazi kipya.Kwa sasa napanga World Rhumba Festival itakayo fanyika hapa Mombasa August mwaka ujao.
safi kabisa ndiye wetu hapa mombasa
ReplyDelete