PATA KUMFAHAMU POUL IBRAHIM KWENYE ULINGO WA MODELING.
Pwani Usanii: Jina lako wajulikana kama nani? Poul Ibrahim:Poul Ibrahim PU: Tueleze kiasi kuhusu maisha yako ya utotoni. Poul Ibrahim:Nilizaliwa Likoni,mitaa ya Kiwerera pale Karibu na flats. Nikasomea Likoni Muslim primary na kujiunga na Pwani secondary school. Hapo ndipo nilianza kufanya uigizaji kwenye tamasha za drama na music. PU:Vyema kabisa. Katika uigizaji labda ulipendezwa na nini? Poul Ibrahim: Nilipendezwa sana na vile nilivyokua najieleza mbele ya umati na vilevile nilikua dancer mkali sana. PU:Na labda ulianza lini mambo ya modeling? Poul Ibrahim: Modeling nilianza high school ila sikua serious serious sana hadi nilipomaliza shule kwa sababu ya masomo. Nilipomaliza masomo hapo ndipo nilipojimwaga uwanjani. PU: Wewe kama model wa kiume umefanya mambo kama yapi? Poul Ibrahim: Nimekua kwenye mashindano na tamasha tofauti za modeling na vilevile nishakua kwenye advertisements za kampuni moja-mbili hivi. PU: Lengo lako kuu hasa ni nini? Poul Ibrahi...