NILIWAPA NAFASI MKAPUUZA,SASA WACHENI NIFANYE KAZI MUONE MATOKEO-KAULI YA PRODUZA KHALID KWA A MILLION STAR SEARCH.


A Million records chini ya Produza Khalid ukipenda Eric Bizzo ilianzisha tamasha la kutafuta wasanii na baadhi ya watu hasa washika dau wa sanaa hapa pwani walilipinga tamasha vikali.(Nadhani kwa sababu ya wivu). Leo Khalid ameamua kupasua mbarika kuhusu mipango yake ya A MILLION STAR SEARCH............
"Khalid Produza
Ati A Million Star Search ilienda wapi?
Nilipokuja na idea ya A Million Star Search watu wengi kutoka hapa Mombasa walidharau na kukejeli kama kawaida yao. Kitu hawakujua ni kuwa nilikuwa nimetenga one million shillings za hiyo Star Search. 250k mshindi, 150k wa pili na 100k mshindi wa Tatu. Advert ya radio nililipa 150k ndio ikuwe mentioned everyday, judges walitoka Nairobi na host, wasanii waliokuwa wakiperform kama Dazlah, Sudi, Susumila wote walilipwa. Advert za banners, posters and other logistics zili cost sana. Chenye nilitaka ilikuwa real talent coz I know how to turn talent into money. Wengi mukaanza kejeli mbona nisim sign Sis P Kwanza ndio nitafute mwengine. Turn out club ilijaa fans but not participants, walikuja kulewa na ku have fun na kuangalia wasanii but si kuingia Star Search. May be kwa sababu ya dharau, pengine ujinga au hawakujua wanachokosa. Less than 10 people participated in A Million Star Search though club zilifurika South coast na Voi. Hawa wote talent zao zilikuwa chini sana.Kulikuwa na maeneo mengi sikwenda kama malindi, mariakani mombasa town na kwengineko, Since pressure ilikuwa imezidi ati nimfanye Sis P superstar Kwanza. ikabidi nisitishe Star Search kwa muda nimfanye kweli Superstar. Sasa bado safari ndio yaanza, Kuna international collabos nyingi nimempangia, tour na shows December na mengi mazuri tu. Haya yote ilikuwa nimfanyie mshindi wa A Million Star Search. lakini bado nitawapa fursa nyengine mwaka ujao. Kila mwaka nitakuwa na sign msanii mmoja kwa A Million Star Search kando na kumpa 250k. Wale washiriki wa mwaka Huu, mwaka ujao nitawapa kipaombele, nitawajumuisha na Wale wapya. Nadhani saa hii mnapiga kelele mkiuliza kwa sababu mshajua ninachoweza kufanya... I think you should know people.... Tuonane mwaka ujao kwa A Million Star Search. Ni hayo tu kwa sasa."

JE KUNA MTU ANA JAMBO LA KUSEMA????

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA