SUSUMILA AFUNGA HARUSI NA MUIGIZAJI KIBIBI.
Msanii gwiji wa hapa pwani Yusuf Kombo almaarufu Susumila leo hii
amefunga harusi na mpenzi wake wa dhati kwa jina Kibibi. Susu anayevuma
kwa kibao TULIZA NYAVU aliachana na mke wake wa kwanza hivi majuzi na
yaonekana ameamua kuchukua mkondo mwingine wa maisha kwa kumuoa
muigizaji Tina aliyevuma kwa kipindi cha K24 TV kwa jina SUMU akiwa
mwanawe Benjamin Kidjo. Twawatakia kila la kheri MR and MRS YUSUF.
Comments
Post a Comment