TEACHER DONDE SAMORA FOR EDUCATION!!! KUMBE MTANGAZAJI DONDE SAMORA MWALIMU???


Ni mtangazaji wa pilipili fm,mlezi wa vipaji,mcheshi,muigizaji na hivi sasa ni mwalimu ukipenda waeza muita kwa jina lake mpya TEACHER DONDE.Mtangazaji huyu mwenye tajriba kuu kwenye tasnia ya sanaa ya pwani tulimpata maeneo ya Junda akifundisha wanafunzi.Donde alionekana mchangamfu na mwenye furaha sana huku wanafunzi wake wakishangilia na kujibu maswali kwelikweli.Tulitengeza kikao ili tuweze kujua zaidi kuhusu teacher Donde na alitueleza hivi........Kwanza napenda sana watoto na elimu.Shule hii ninyofundisha inaitwa Junda Bright Academy. Nafundisha Science,English,Soci­al Studies,Kiswahili na Hesabu.Class 4 na 5.Huwa ni furaha sana pale tunapokuwa darasani.Masaa yangu ya kufundisha huwa sanasana ni jioni.Mke wangu pia ni director na ni mwalimu papa hapa Junda Bright Academy.Kitu watu hawafahamu ni kuwa nilisomea Education chuo kikuu."
Tulimuuliza Donde Samora vile yeye ni mcheshi na anapenda mzaha je wanafunzi humskiza kweli ama ni kumchezea humchezea??Donde alituambia hivi......"Watoi wanasikiza sana na wakileta mchezo wanapokea kichapo kiasi."
‪#‎TEAMPWANIUSANII‬ twasema heko teacher Donde!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA