HIPHOP HEAVYWEIGHT HUSTLA-JAY AWASHIRIKISHA WASANII WATOTO KWA WIMBO WAKUTUKUZA WANAWAKE.
Baada ya kutoa video 'Intercontinental scar' msanii Hustla-j aliyesajiliwa ndani ya S3 studios Nairobi amezuka upya.
Hustla-Jay alipangiwa project hii na msanii Babaluku na kukutanishwa na wasanii hawa wachanga ili aweze kuwashirikiana nao. Wasanii hawa wadogo wanaotoka nchi jirani ya
Uganda wakiwa na Babaluku na Hustla-Jay wamelenga mada inayopuziliwa sana na wasanii.
Ushirikiano huu umempa mwanamke wa kiAfrika kipao mbele huku mila na tamaduni zikiwadhalilisha.
Wimbo wenyewe unaitwa 'Amandla' {power to the women} Hustla-Jay akiwashirikisha Babaluku toka Uganda,Mc flower aliye na umri wa miaka 13 kutoka Uganda na Khamara Ashnan poet 16 kutoka Uganda. Project hii iliandaliwa na Gwiji wa miondoko ya hiphop anayetokea Uganda,Babaluku. Project hii ilyofanywa nchini Uganda iliangazia vipaji kwa vijana hasa kandanda,ushairi na muziki.Tayari video ya wimbo huu ipo kwenye maandalizi.
Comments
Post a Comment