JE WAMFAHAMU KASSIM MBUI??? MTANGAZAJI WA PILIPILI FM ALIYEJITOLEA KUWASAIDIA CHIPUKIZI
Kipindi chake cha MisheMishe za maisha PILIPILI FM kila jumapili usiku kimesaidia na kutambulisha vipaji vingi hasa vya sanaa hapa pwani. Ndiposa hatukuwa na budi kumtafuta ili atueleze safari yake ya kuenua vipaji ilianza wapi,vipi na imefikia wapi.
Kassim Mbui aeleza.........
Nafahamika kwa jina kama Kassim Mbui.Mzaliwa wa hapa pwani,kwa sasa nina umri wa miaka 23 mwaka huu Inshallah nitagonga 24.Kitaaluma mimi ni mwanahabari nimesoma na nikahitumu pale TUM(Technical University of Mombasa) mwaka wa 2013 baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka wa 2009 katika shule ninayoienzi kwa sana St Georges High school.Kazi ninayoifanya kwa sasa sio kwamba nakosea njia ila ni kitu nilichikuwa nacho nikiwa na umri mdogo sana.Wakati huo nikiskia watu kama kina George Biff Mkuzi,Omar Mwagao,Papah Mukulu,Donde Samora na wengineo.Nilitamani sana angalau pia mimi siku moja niwe naeza nikasikizwa kama hivyo. Passion yangu ya kutaka kuzungumzia maswala ya jamii itimie.Kwa sasa nina furaha sana wengine bado nawaskia na wengine nafanya nao kazi kama Donde samora,mtu ninaye mheshimu kwa sana.
Kuingia kwangu kwa redio haikuwa rahisi ila bidii,maarifa na kujituma zaidi.Nilianza kufanya kazi nikiwa semester ya pili campus.Na hivi ndivyo ilivyokua......
Nilitolewa class nikiwa na mwenzangu Ibrahim Nyundo ambaye ni rafiki na kama ndugu tukiwa campus kwa sababu tulikua twadaiwa fees.Kwa hiyo, tulipotolewa ikabidi the whole two weeks tuwe nje.Tukasuggest kutuma application,by that time PILIPILI FM ilikuwa imefunguliwa na ilikua na one month. Tulikuja mpaka pilipili fm na kwa bahati nzuri tukapanda na director kwa lift.Akatuulizwa mwaenda wapi,tukamwambia twaenda pilipili fm kutafuta kazi.Akatuuliza nani amewaambia kuna kazi? .Tukamwambia tunaenda bahatisha akasema sawasawa.Tulipofika juu tukaweka barua halafu general manager by that time akatuita akatuuliza maswali. Tulimsifia na kumwambia unatuhitaji sisi na tutamfanyia kazi poa.Alituamini na kujua vijana wako poa.One week later tukaitwa na tukaanza kazi huku tukiendelea na class.Hivyo hivyo hadi tukanyooka na kuwa hodari mpaka tukaanza fanya programes tofauti.
Baadaye nilikua sana na malengo ya kuinua vipaji hasa vya wasanii chipukizi kwa maana walikua wengi wanalilia sana airplay. Kwa hio, I thougt vile niko na nafasi hiyo,let me try my level best nione tutasaidiana ki vipi.
Nikiwa host na mwenzangu Sophia Saidun katika kipindi mishemishe za maisha.Lengo kuu likiwa kuzungumzia maisha ya kila siku katika jamii.Lakini I had to write proposals for two more hours kwa ajili ya ajenda niliyokua nayo ya kusaidia wasanii chipukuzi ila tukaamua tuifanye tofauti sana.Badala ya kucheza ngoma tukaonelea every Sunday tunakua na msanii anayeibukia ila anajituma na ana malengo.Mbali na msanii pia na producer tukakuta poa ili kutoa ile lawama ya msanii kafanya kitu kibovu aseme ni producer..Pia producer afanye kitu kibovu aseme ni msanii hajijui.Ndiposa every sunday tunakuwa na msaani chipukizi though kipindi kina vipengee tofauti but music tunayo play ni ya wasanii ibukia.
La msingi nawahakikishia vipaji vipo kwa sana. Vijana wanaimba ila kunahitajika ushirikiano wa dhati kwa kila mshikadau.Mkubwa amsaidie mdogo na sote tushikane mikono ili tusaidiane.Hakuna mwanzo rahisi,hii ni ya wasanii wanaoibukia nothing comes in a silver plate lazima ujitume.
Comments
Post a Comment