TAFSIRI YA WASANII KUMI WA PWANI WATAKAOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA HUU.
10.Ziky wa Ziky
Ni msanii mchanga aliyesajiliwa ndani ya Jungle Masters chini ya produza mkali Emmy Dee. Ziky wa Ziky amethibitisha uwezo mkali kwa wimbo wake wa kwanza na kuichukua style ya wanamuziki wa Jungle Masterz vilivyo, kama vile Dogo Richy, Majid na Lypso . Tarajieni makubwa kutoka kwa Ziky wa Ziky.
9.SHEMBWANA MASAUTY
Msanii huyu alidhihirisha uwezo wake kwa wimbo 'uko mbali' ambao japo haukuvuma sana hivyo ulimleta karibu na mashabiki zake. Baada ya hapo chini ya Liwazo records,Shembwana alirudi kwa kibao cha dancehall 'siwezi' kilichomtambulisha Kenya nzima na kumvutia mashabiki chungu nzima. Mwaka huu, twahisi Shembwana atakuwa moto wa kuotea mbali na twatarajia burudani la kukata na shoka kutoka kwake.
8.KIWANJA
Ni dhahiri shahiri kuwa Malindi kuna vipaji na bila shaka tunamzungumzia msanii Kiwanja. Rapper huyu chini ya Malindi records amezuka vikali kwa vibao vyake 'Afrikano' na collabo kali kwa jina 'bonde chafu'.Vibao hivi vinamuweka msanii Kiwanja juu na bila shaka hatupingi kuwa mwaka huu atakuwa miongoni mwa watakao peperusha bendera ya sanaa ya pwani juu zaidi.
7.P-DAY
Anapendwa na wengi kwa mtindo wake wa kuchanganya lingala na fleva za kimwambao na mashabiki bila shaka hutaka zaidi kutoka kwake. P-day ambaye mwaka huu ameshika sanaa ya pwani kwa vibao kama 'nylon guitar' na 'sweetie' mwaka huu ni wake kwa sababu ana mipango kabambe ya kushirikiana na magwiji wa lingala na kutuangashia vibao vitakavyo wafanya mashabiki washeki legiii!
6.CHIKUZEE
Mwaka uliopita Chikuzee alivuma sana kwa ushirikiano. Kupitia Rapdem, Flim-C, Susumila na Chege msanii huyu alijitwika jukumu la mfalme wa collabo kwani mwaka huu pia ameshafanya collabo akishirikiana na Dazlah, Busy-K na wengineo. Hivyo basi nyota yake itazidi kung'aa kwani wasanii wengi wanahitaji msaada wake ili waweze kusimama.
5.SIS P
Japo alitoa vibao viwili tu mwaka jana, Sis P alipata wafuasi wengi Kenya nzima na kulijenga jina lake vilivyo. Binti huyu amezoa sifa kibao sio pwani pekee bali hata Nairobi kwani hatuwezi sahau kuwa ndiye best female artiste of the year!
4.Sudiboy
Sudiboy amepiga muhuri na kutuhakikishia kuwa ndiye mfalme wa muziki wa Pwani. Sudi amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wakali Nairobi wakiwemo Rabbit, Cannibal na Amileena.
3.Kaa la Moto
Mkali wa vina na mashairi alitamba kwa vibao kama mia kwa mia ambayo video yake ilienea sana. Vilevile yupo kwenye wimbo 'mapanya' ya Nyota Ndogo. Hakuna maneno mengi hapa kwa Kaa la Moto. Amekubalika tayari.
2.Susumila
Kwa kweli kama kuna msanii amefanya bidii sana mwaka huu, basi hatuna budi kusema ni Susumila. Amefanya show zaidi ya nyingi huku vibao vyake 'ngoma itambae' na 'hidaya' kuzoa mashabiki Kenya nzima.Tusubiri mwaka huu.
1.HUSTLA-JAY
Ni rapper mkali ambaye wimbo wake wa 'continental scar' ulitamba sana kumfanya awe mmoja wa wasanii wa Kenya kuchezwa Channel O. Hustla, chini ya Sandstone Studios amefanya project kalikali Afrika mashariki huku video zake zikiwa za gharama na za hali ya juu sana. Amejitwika jukumu la kubeba sanaa ya pwani na kuifikisha Afrika nzima. Tunaweza sema kuwa Hustla-jay anayo mipango bam bam ya kufika mbali mwaka huu kwani tayari ameshirikiana na wasanii wa Afrika mashariki kwa ujio wake mpya. Hivi majuzi alikuwa nchini Tanzania ambapo alifanya Collabo na msanii Ibra Da Hustla.
Tegea.
Comments
Post a Comment