PATA KUMFAHAMU MTANGAAJI GWIJI 'ATHMAN AYUB MATUMBO' BABA MLEZI WA SANAA YA PWANI AKIELEZEA SAFARI YAKE KWENYE JUMBA LA UTANGAZAJI.
(Akielezea mwenyewe)
Nilimaliza elimu ya msingi 1993, pale Dabaso primary school, Watamu.
Nilifanikiwa kuibuka mwanafunzi bora mwaka huo katika eneo lote la Gede na nikapata nafasi ya kujiunga na shule ya upili Godoma Boys.
Kutokana na hali ngumu ya maisha fedha ilikuwa shida nilishindwa kuendelea na masomo Ya upili Godoma na nikahamia nchi Jirani ya Tanzania ambako nilibahatika kuendelea na masomo yangu hadi kidato cha sita pale islamic seminary school ya ununio boys.
Lakini Kila jambo lina sababu yake baada ya kuhamia bongo ,miaka hio ndio muziki wa bongo flava ulikuwa inazaliwa.Kipindi hicho mziki huo ukiwa unaitwa BONGO ZANIA.Niliweza kushuhudia mwanzo wa mziki huu wakati huo wahasisi wakiwa ni kina Swaleh Jabri, Nigga One, Kyadaman, Ras Pompidu. Ndipo wakaja kina Too Proud a.k.a Mr TWO au Suguu Nigga Jay kwa sasa Profesa Jay.
Nami sikuachwa nyuma kwani nilikuwa ni mwanamziki wa kufoka foka, hip hop artist Japo sikuwahi kurekodi.
Baadhi ya wanamuziki ambao tulikuwa tukifoka shuleni lakini baadaye mziki ukawakubali ni pamoja na Hamis Mohammed Mwinyinjuma a.k.a Mwana Fa ambaye tulikuwa shule pamoja, Hekima Asilia and The Bongo Flava, ambaye mimi na yeye tuliunda kikundi chetu cha hip hop. Kwa sasa Hekima na The Bongo flava yuko nchini uingereza anaendeleza muziki kimataifa.
Utangazaji ulikuwa ndoto yangu tangu sijaanza chekechea, wazazi wangu walikuwa na ada ya kusikiliza Idhaa ya kiswahili ya Ujerumani.Nilitamani sana kuingia nami redioni kuanzia kipindi hicho, kwa hivyo Chochote nilichokuwa Nikifanya lengo nifike utangazaji.
Hakuna kazi niipendayo hapa duniani zaidi ya uwana habari, hio ndio taaluma yangu, na naipenda sana kazi yangu.
Ndani ya kazi yoyote ile ni lazima upitie changa moto.Mtangazaji ni kama balozi unawakilisha jamii, hivyo basi kama kioo cha jamii .Jamii yategemea uwe karibu nao, na habari uzitowazo zisiegemee upande wowote.
Na changamoto nyengine ni ukiwa mtangazaji uhusiano wako wa kimapenzi unaweza kuvunjika iwapo mwenzio hatokuwa mvumilivu.
Labda jambo moja nilisahau kueleza ni kwamba ndani ya malindi city nilisha fanya kazi nyingi tu ya kuendeleza usanii pwani ni vigogo kama vile Mbuyu wa Tabaka, Majizee na hata pia producer Easy Jay na Saint P,ambao tulikuwa tukijifunza kazi ya kutengeza muziki wa kizazi kimya chini ya Undaa a. K.a.mitaa kisauni.
Ndoto yangu kubwa ni kuendeleza vipaji vya wasanii pwani,ambapo mimi kama radio presenter ndiye niliyekuwa mtangazaji wa kwanza kupeperusha vibao viwili vilivyo mtambulisha msanii Sudi Boy, banati na nzaro. Pia msanii Mr Bado nilimtambulisha hewani baada ya kugunduwa anauweza mziki,ni wasanii wengi sana wakiwemo kina Ally B na Dr . Malik.
Mwisho najua mashabiki wamenimiss sana ila elimu muhimu, naongeza elimu kidogo nchi za nje, ili nikirudi nitimize ndoto zangu kuinua vipaji vya wasanii pwani.
Swadakta Bro
ReplyDelete