KUTANA NA DEEJAY BADAGAH.....AKITUELEZA KUHUSU BEAT YAKE....ANAYEJULIKANA NA WENGI PWANI!!!


PWANI USANII:YOH KARIBU SANA.TUAMBIE JINA LAKO. 
BADAGA: Jina langu ni Ali Khamisi Badaga .
 
PU: UNATOKEA PANDE GANI YA PWANI?
BADAGA: Mi ni mzaliwa wa Kongowea na mkaazi wa kongowea.

 
PU:TUELEZE KUHUSU FAMILIA YAKO KIDOGO:

BADAGA:Wazazi wangu wawili Badaga na mishi pia ni wakaazi na wazaliwa wa papa hapa Kongowea. Kabila yangu ni mdigo family ya Ali from Golini Kwale alipotoka Makwere Ali .Jina la Ali limetoka kwa mzee aliezaa babu Ali, alieza babake Makwere Ali na Ali wengine kwa family,

PU:SHWARI KABISA.SASA TUELEZE KUHUSU MAISHA YAKO KWENYE TASNIA YA MUZIKI:
BADAGA: Kabla Badaga nilikua najiita Small G. Hapo ilikua ni msaani kuhustle hapa na pale jina lilipanda but mavuno hakuna akabidi niwe dj mtaani huku nikijifunza music production jioni kwenda mafundisho kuimba na jirani yangu dada aliyeimba kiatu kivue mpaka nilipoitwa studio mwaka 2001.
 

PU:ENHEE KISHA.........
BADAGA:Niliendelea na mziki hadi kurekodi Anastacia single mbili but hazikwenda hewani zilienda sokoni moja kwa moja, kazi nyingi nzuri nilifanya but zilikua sokoni.
Siku moja ilitokea kutoelewana meneja wangu nikaamua kuwacha kufanya kazi kwake na kuanza kazi na dj Wizard Tuffgong wasanii recordz.

 
PU:JINA BADAGA NI MAARUFU SANA.JE LILIKUJAJE?
BADAGA:Jina dj Badaga halikuja kiurahisi, palitokea msanii kwa jina lilo hilo. Pwani f.m ikampa shavu sana ikabidi mimi pia
nitumie real name. Hapo ndipo kazi ilipoanza hadi kumtoa msanii kama Escobar,Mtu saba,Black machizi,Mtu PK,Swang na wengine wengi.

 
PU:TUELEZE JINSI ULIVYOANZA KUREMIX NYIMBO ZA WASANII:
BADAGA:Mwaka wa 2002 na 2003 niliweza weka mkutano na disco zote za pwani na hata za bara ili kueneza muziki wote ulioko chini na kama kweli walikubali kama Omega disco akiwa Nick na Ninja man,Boiz2Men,Rocks sound,Timberland sound,Atomic sound,M.city sound,Lucky sound na wengine wengi sana. 

 
PU:KIPI KILICHOFAUTA?

BADAGA:Kazi ilikua nzuri dj Badaga kujulikana mpaka tukaanza toa mix Tuffgong djz tukiwa compee Stuntmasterz..

 
PU:TUELEZEE KUHUSU STUDIO YAKO YA BLACK RECORDZ:
BADAGA:Baada ya muda kusonga nikaamua kwenda solo hadi kufungua Blaq recodz hadi kumtoa Dogo Richy 'shamba' kumfunza muziki,kumrekodi hadi kumfanyia video mbili kali 'lea' na nyingine 'please Mummy' kupitia usaidizi wa Backstreet hadi leo.
napenda sana muziki na kusaidia wasanii chipukizi na hata Playboy Wynas nimemtoa na wasanii kadhaa wanacheza movie kupitia kwangu zipo kwenye runinga.

PU:LA MWISHO,UNGEPENDA KUWAAMBIA WASANII NA MASHABIKI ZAKO NINI?

BADAGA:Mimi ndio Badaga mpenda talanta

Comments

  1. How can I get your Beats bro

    ReplyDelete
  2. Kuuliza Sasa Hizo Nyimbo zenye Ulifanya Remix Tunaeza zipata kwa platform Gani?

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA