KUTANA NA ACTOR MJ WA KIPINDI CHA ALMASI CHA K24 AKIELEZA TOFAUTI YA MJ NA JUMA SHIBE
Pwani usanii:Je ulianza usanii wa uigizaji lini?
Juma Shibe: Nilianza usanii back when I was in high school:
nikapata 3 awards za best actor coast province.After school nikatia juhudi zangu zote kwa kipaji changu nikapata scholarship ya kusoma video production Nairobi at National youth talent academy for one year.
Pwani usanii:Tueleze kuhusu filamu yako ya kwanza.
Juma Shibe:Nilipomaliza high school is when nilianza my first movie "KIZA" with a group inaitwa Kwale arts.My second movie inaitwa Shimo la tewa nilimshirikisha Chikuzee zote hizi mbili zilionyeshwa pwani tv.Nikafanya nyingine inaitwa Unconditional love yenye iko African magic Swahili na hii ndio ilinipa best actor kwa Coast film festival 2013.
Pwani usanii:Tueleze project ulizofanya mwaka huu.
Juma Shibe:This year ndio nikachukuliwa na Ashiner picture wakanipa role ya MJ.
Pwani Usanii:Tueleze kidogo kuhusu role yako ya MJ kwenye kipindi cha Almasi?
Juma Shibe:Mj kwa Almasi ni kijana aliyeishi maisha ya uchokoraa mpaka alipopata hifadhi ya buda anayejulikana kama Baraza,mj aligeuka na kuwa mjanja wa jiji kwa kuwa alipata pesa nyingi za kazi haramu.Wasichana kwake ni kama chakula lazima apate,kiamsha kinywa,lunch na supper.
Pwani Usanii:Tofauti ya MJ na Juma Shibe ni ipi?Manake watu wengi wanadhani vile ulivyo kama MJ ni vile ulivyo kama Juma.
Juma Shibe: Okay Mj ni womanizer tofauti na Juma ambaye hana story za wasichana.Napata inbox nyingi za warembo wakiwa na matumaini kuwa nitawatongoza ila mie sina mambo hayo kamwe kile hawajui ni kuwa Mj wamemuacha K24.
Pwani Usanii:Tueleze matarajio yako ya hivi karibuni:
Juma Shibe:Natarajia kufanya project zaidi ya moja baada ya Almasi na company ya Ashiner pictures,pia Kuna movie ambayo karibuni nitafanya na company kubwa Tanzania.
Pwani Usanii:Waeza wapa wasia gani vijana wenzako ambao wangependa kujiunga na sanaa ya uigizaji?
Juma Shibe:Safari ya acting inahitaji uvumilivu,bidii na heshima,ukiwa na vyote hivi utafika mbali.
Comments
Post a Comment