BAADA YA SUSUMILA NA KIGOTO.............KAA LA MOTO NA JOHNY SKANI WAJIBIZANA KWA WIMBO MPYA 'HAUNIWEZI.'
Ni hivi majuzi tu pale wasanii Johny Skani na Kaa la moto kiumbe walipokuwa na tofauti ukipenda 'beef'. Produza Amz wa sq records aliwaleta pamoja na kutengeneza beat ya kufa mtu ili wawili hao waweze kufanya kazi pamoja. Japokuwa msanii Kaa la moto alikuwa anakataa offer hio na kukataa kwenda studio mwishowe alikubali na matokeo ni wimbo HAUNIWEZI. Wimbo huo, produza Amz amedhihirisha kuwa ni mkali sana kuporomosha mabeati ya hiphop kiutu uzima. Johny Skani naye alicheza na vina, mizani na maneno vizuri akijaribu kumfunika Kaa la moto vilivyo. Kiumbe naye vilevile kama kawaida amefunika mistari ya kueleweka vilivyo ili aweze kuteka sikio la mashabiki zaidi ya Skani. Cha kushangaza kuhusu wimbo huu ni kuwa ni idea ile ile ya Susumila na Kigoto 'UBISHI' ila raundi hiii imekuja kimtindo mwingine. Mashabiki ndio watakao amua!!!!!!
Comments
Post a Comment