NILIWAPA NAFASI MKAPUUZA,SASA WACHENI NIFANYE KAZI MUONE MATOKEO-KAULI YA PRODUZA KHALID KWA A MILLION STAR SEARCH.
A Million records chini ya Produza Khalid ukipenda Eric Bizzo ilianzisha tamasha la kutafuta wasanii na baadhi ya watu hasa washika dau wa sanaa hapa pwani walilipinga tamasha vikali.(Nadhani kwa sababu ya wivu). Leo Khalid ameamua kupasua mbarika kuhusu mipango yake ya A MILLION STAR SEARCH............ "Khalid Produza Ati A Million Star Search ilienda wapi? Nilipokuja na idea ya A Million Star Search watu wengi kutoka hapa Mombasa walidharau na kukejeli kama kawaida yao. Kitu hawakujua ni kuwa nilikuwa nimetenga one million shillings za hiyo Star Search. 250k mshindi, 150k wa pili na 100k mshindi wa Tatu. Advert ya radio nililipa 150k ndio ikuwe mentioned everyday, judges walitoka Nairobi na host, wasanii waliokuwa wakiperform kama Dazlah, Sudi, Susumila wote walilipwa. Advert za banners, posters and other logistics zili cost sana. Chenye nilitaka ilikuwa real talent coz I know how to turn talent into money. Wengi mukaanza kejeli mbona nisim sign Sis P Kwanza...