TAFSIRI YA WASANII KUMI WA PWANI WATAKAOFANYA VIZURI ZAIDI MWAKA HUU.
10.Ziky wa Ziky Ni msanii mchanga aliyesajiliwa ndani ya Jungle Masters chini ya produza mkali Emmy Dee . Ziky wa Ziky amethibitisha uwezo mkali kwa wimbo wake wa kwanza na kuichukua style ya wanamuziki wa Jungle Masterz vilivyo, kama vile Dogo Richy, Majid na Lypso . Tarajieni makubwa kutoka kwa Ziky wa Ziky. 9.SHEMBWANA MASAUTY Msanii huyu alidhihirisha uwezo wake kwa wimbo 'uko mbali' ambao japo haukuvuma sana hivyo ulimleta karibu na mashabiki zake. Baada ya hapo chini ya Liwazo records ,Shembwana alirudi kwa kibao cha dancehall 'siwezi' kilichomtambulisha Kenya nzima na kumvutia mashabiki chungu nzima. Mwaka huu, twahisi Shembwana atakuwa moto wa kuotea mbali na twatarajia burudani la kukata na shoka kutoka kwake. 8.KIWANJA Ni dhahiri shahiri kuwa Malindi kuna vipaji na bila shaka tunamzungumzia msanii Kiwanja. Rapper huyu chini ya Malindi records amezuka vikali kwa vibao vyake ' Afrikano ' na collabo kali kwa jina 'bo...