SOKORO BADO YUPO NA AMESHIRIKIANA NA RABBIT KWENYE WIMBO MPYA!!
Mara ya mwisho kumsikia hewani ni enzi za Tabasamu records akiwa kwenye wingu la umaarifu wa sanaa Afrika mashariki. Baada ya kimya kilichozua maswali mengi yaliyojiri ni gwiji wa hiphop Mombasani Sokoro yupo Rehab ya madawa ya kulevya kihali maututi.
Baada ya kupitia kwenye mikono ya matibabu ya rehab Sokoro alirudi tena na kusikika hewani kwenye show tifauti za muziki hasa ile ya Mashavmashav pwani fm. Juzi alikuwa na show maeneo ya Likoni, Jetbar resort. Leo hii tumewasiliana na Sokoro ili kumjulia hali na mipango yake kwenye ulingo wa sanaa. Sokoro alitueleza hivi.......
"Nashukuru sana mashabiki wangu sugu wale wamekua nami tangu enzi ningependa wajue niko bora kiafya."
Kuhusiana na hali ya muziki wake Sokoro alitueleza hivi..........
"Nimefanya ngoma mpya Nairobi na RABBIT,BLACK JESUS,SINGER AFRICANA and my new music video WANAULIZA ULIZA is in the pipeline coming soon, it's COAST HIPHOP forever."
Kwa mashabiki wa hiphop na wa Sokoro msife moyo,msanii wetu bado yupo sana na buheri wa afya kabisa.
Comments
Post a Comment