MISS TOURISM MOMBASA YASHINDWA KULIPIA MAVAZI YA WAREMBO
Tamasha kubwa ya Miss Tourism Mombasa ambayo ilifanyika siku ya jumamosi usiku ndani ya Wild waters ilipatwa na changamoto la aibu pale waandalizi waliposhindwa kulipia costume ambazo Warembo walifaa wajishebedue nazo kwenye jukwaa katika kitengo cha mlo wa jioni. Warembo hao walilazimika kutumia nguo zao tofauti tofauti kwenye jukwaa manake hawakua na budi. Yadaiwa mshonaji mashuhuri wa nguo hizo ambaye ni mchumba wa msanii King Sting alidinda kupeana nguo hizo manake alikua hajalipwa lolote na wala hakutaka kusikia hadithi eti atalipwa hela baada ya show. Hali hio ya ukosefu wa hela yadaiwa ilichangiwa pakubwa na kutojihusisha kwa serikali ya kaunti ya Mombasa katika tamasha hio. Hakuna mwakilishi yeyote kutoka katika serikali ya Kaunti ya Mombasa ambaye alihudhuria. Wageni mashuhuri waliohudhuria ni mbunge wa Nyali Hezron Awiti na Mwenyekiti wa Bandari ya Mombasa bwana Danson Mungatana.
Story and picture Courtesy of Backstreet Entatainment
Comments
Post a Comment