EXCLUSIVE INTERVIEW MEET WYNAS PLAYBOUY:


Pwani Usanii:Tuambie majina yako kamili.

Wynas PlayBouy:Kwa majina kamili naitwa..Willy Mnao Msya..hapo Ndio Jina Langu La Mziki Lilipotokea Wynas.

PU:Ulianza muziki lini?

Wynas:Muziki Wangu Nlianzia Kwa Lai,crack Sound Wakati huo Nikiwa Kwa Kikundi Kilichoitwa Nicknemz.Mwaka Wa 2009 kundi Lilivunjika Mwaka Wa 2012 ambapo niliamua Kusimama Kama mimi Wynas..sikufa Moyo"niliamua Kufanya Mziki Kivyangu.

PU:Muziki peke yako ulianza vipi?

Wynas:Nilizamia Kwa Badaga Ju Hela Ya Studio Kubwa Haikupatikana Kwa Uraisi..na hapo Ndipo Nyota Yangu Ilianza Kung'aa Baada Ya Kuachia Nyimbo Kwa Jina Mchizi Masu Ambayo Ilishika sana Street.baada Ya Watu Kunipongeza Na Kuniamini Niliamua Kwenda Studio Kubwa Ili Nitimize Ndoto Yangu.

PU:Uliingia Studio ya Tee hits lini?

WYNAS:Nilihamia Tach Za Miba 2012 Mwezi Wa Nane.

PU:Wimbo wako wa kwanza ulikuwa upi chini ya Tach za Miba?

WYNAS:Ngoma Yangu Ya kwanza Chini Ya Tee Hits Iliiitwa Roho Mbaya Ambayo Haikushika Vizurii ila Sikufa Moyo.nilirudi Tena Na Kuachia Kete Kwa Jina Mabeib Ambayo Nilimshirikisha Dazla ambayo Ilifungua Milango Ya Baraka Kwenye Muziki Wangu Ju Watu Waliipenda Na Pia Ilipata Kuchezwa Kwa Vituo Vya Radio.

PU:Nyimbo gani zilifuata?

WYNAS:Baadaye niliachia UNANIONEA,­FALL IN LOVE,PLAYBOUY,RUDI,NA­NI NDIO NANI na PENZI U TURN Ambayo nilimshirikisha SHAABIGGY ambazo Ni Ngoma Zimekua Zikisumbua Chart Za Coast na hata Nairobi.
PU:Tueleze kuhusu kibao chako cha PLAYBOUY ambacho kimevuma sana.

WYNAS:Kwa Kuimba Kibao Cha Playbouy Ambacho Nimezidi Kunipa Sifa Watu Waliamua Kunibadilisha Jina Na Kuniita Playbouy Badala Ya Wynas...na Pia Playbouy Ni kibao Ambacho Kimesumbua sana Hadi Bongo.

PU:Una mipango gani ya muziki hivi karibuni?


WYNAS:Mipango Yangu Kwa sasa Ni Collabo Kubwa Ambayo Inanukia Ambayo Nitafanya Na Msanii Kutoka Bongo..ila Jina Ntalibana Kwa sasa,kuna Ngoma Mpya Ambayo nitaichia Ngoma Kwa Jina TUJIRUSHE. Hiyo Ni Baada Ya Kuimba Mapenzi sana.

PU:Swali la mwisho. Je Una mpenzi?

Wynas:Sina mpenzi mimi Ni Playbouy.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA