RAPPER HUSTLA JAY AKAMATWA NA POLISI KWA KUWA MLEVI!!
Msanii gwiji wa hiphop Hustla Jay alijipata pabaya Jumanne iliyopita pale aliposhikwa na polisi wa kitengo cha trafiki baada ya kupatikana yeye pamoja na rafiki zake wakiwemo rapper Fikra Teule na Euticus Otieno. Watatu hao waliokuwa wanatoka mkahawa wa Sheba Lounge kuelekea nyumbani huku dereva akiwa Euticus walipigwa na butwaa pale polisi walipowakamata na kuwatoza faini ya Alco-blow.Kando na hayo watatu hao walishukiwa kuwa walikuwa wavutaji bangi ila Hustla Jay alidai kuwa ni Cigars.
Baada ya kutoa faini hiyo Hustla Jay na rafikize waliwachiliwa huru.
Comments
Post a Comment