PRODUCER MSANII LAI ATIRIRIKA HUKU AKIMSHIRIKISHA KIDIS KWENYE UJIO MPYA!!!
Huku akiwa bado wimbo wake special alioutoa mwezi wa Septemba umekita na kushikilia chati za muziki wa pwani,msanii ambaye vilevile ni producer gwiji tokea Kilifi amerudi tena kuangusha ujio mpya kabisa. Raundi hii Lai amemshirikisha msanii Kidis the Jembe.
Tuliwasiliana na LaiLai na akatueleza hivi kuhusiana na wimbo wake mpya.
"Track mpya nimefanya na Kidis inaitwa Tiririka nimeachilia on sunday, yenyewe najua tayari nina trck nilifanya na chikuzee ambayo tayari inafanya vyema na kushikilia number 1 katika chart kadhaa za mziki lakini nimeamua kuachilia Tiririka pia kama njia ya kupata mauzo,downloads na shows zangu."
Tulimuuliza Lai kuhusiana na tabia yake ya kufanya collabo kila mara na alitueleza hivi............."Kuhusu kufanya collabo mingi,yes kwangu mimi collabo or no collabo,kile najali zaidi ni mashabiki wamepata Mziki mzuri tu na hio nimeidhihirisha katika Tiririka....."
Tegea pwani usanii upate kutiririka zaidi.
Comments
Post a Comment