NYOTA NDOGO AONGEA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MZUNGU BAADA YA KUINGILIWA KWA MANENO MITANDAONI!!
Ni juzi tu pale msanii Nyota Ndogo alipovunja mbarika na kutangaza
asmi penzi lake la miezi tisa na mchumba wake wa kizungu kwa jina Henning Nielsen.
Kilichofuata ni maneno ya watu kwenye mitandao ya kijamii kumuingilia. Wengi wao wakimpa kongole na kumtakia mema na kila la heri kwenye uhusiano wake ila baadhi ya watu walikereka na kumsuta kwa maneno mabaya msanii Nyota Ndogo.
Akihojiwa na Manuel Ntoyai editor wa Spice Magazine, linalopatikana ndani ya People Daily, Nyota alidai kuwa anashangaa sana kwa wanaokereka kwani yeye pia ni mwanamke na anahitaji raha zake bila kuogopa yeyote. Japokuwa hakutaka kuyaweka mapenzi yake wazi hapo mwanzoni, aliamua kutamngaza rasmi ili kila mtu atambue kuwa amepiga hatua pande ya mambo ya mahaba.
Habari ndiyo hiyo.Twamtakia kila la kheri.
Comments
Post a Comment