WASANII WA PWANI WANATUMIA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA? pata ukweli hapa
Ni dhahiri shahiri kuwa lisemwalo lipo na kama halipo laja. Story na visa vingi vya kurogana na kuenda kwa mganga katika sanaa ya pwani vimetambaa na kuenea mitaani. Japokuwa sio wote wanaokubaliana na kasumba hizi ni juzi ambapo msanii Majid kule kule wa jungle masters alipokuwa mgonjwa hali mahututi na lililofuata ni watu kusema kuwa karogwa na msanii mwenzake, tena rafiki yake wa karibu. Vilevile tusiwasahau Sokoro na Pharaoh watu waliongea sana kuhusu hali zao na baadhi ya wengine kudai waliendewa kwa waganga. Jana katika kipindi cha Radio kaya kinachoitwa CHIPKIZI ZA KAYA mada hii iliongelelewa kwa kina na wengi wa mashabiki wakijitokeza kuchangia. Mada yenyewe ilikuwa hivi -Uchawi, Uganga .... etc. Je ni ukweli ushirikina upo katika tasnia ya mziki pwani...? Je ni kweli katika karne hii ya 21 bado kuna baadhi ya wasanii wanaomini kutoka kimziki mpaka uende kwa babu?- Tukinukuu kutoka kwenye ukurasa wao wa facebook,baadhi ya watu walitoa maoni kama haya.
David Giize "uchawi upo kwa wingi,mwanzo hakuna wachawi wakubwa ka wasanii,coz kila mtu anataka kuwa juu kuliko mwenzake"
Ali Kunyetta "C unajua kaz bila dawa haiwezekan,ivo basi uchawi upo tena sana,"
Lucas John "Kaka uchawi upo,kwa mfano wewe umtangazaji alafu mtu hakuonei raha itabidi uende kwa mganga ukajifungue na huo utakuwa ni uchawi"
Dogo K Mkali Kwanza "Mimi naeza sema mtu anaesema kuna uchawi huwa ni mshiriki wa mambo hayo kwasababu huwezi sema2 shann ananiroga ukiwa huja shiriki kwahio nasema wasanii wakaze buti kisawa sawa wachane na mambo ya kushiriki"
Jemo'c Danga Lao "Ama Kwa Ufupi Mshirikina Atabaki Kuwa Mshirikina Kwa Jambo Lolote Lile, Nae Mja Mchamungu Vilevile Atamuomba Jalali Bla Ya Kizizi"
SWALI NI JE WASANII WA PWANI WANATUMIA NGUVU ZA UCHAWI NA UGANGA?
Comments
Post a Comment