KIGOTO MMBONDE ANOGA KIMAPENZI!!
Mkali wa mafleva ya RnB na afro-fusion na aliyekubalika na wengi sio mwingine bali yuleyule Kigoto Mmbonde ametangaza msimamo wake rasmi kuhusu maisha yake ya mahaba. Mshikaji huyu ametiririka hisia zake katika wimbo wake mpya NIPENDE. Kigoto ameandamwa na scandal nyingi za mahaba hivi karibuni ndiposa akaamua kujieleza kupitia muziki. "Wimbo mpya nimefanya hornet chini ya producer TK2 ngoma yaitwa nipende. Halafu vilevile mashabiki wawe tayari kwa video mpya ninayoitoa karibuni ya goma langu la ridhika," alitueleza Kigoto.
Comments
Post a Comment