KINGSTING NA BEDBUG WARUDI TENA KIMUZIKI!!!!
Je mnakumbuka enzi za nyimbo #sonai na #anisa ? Nyimbo hizo zilizopamba moto enzi hizo mpaka sasa, zililetwa kwenu na wasanii wakali Kingsting na Bedbug. Baada ya hapo kimya kirefu kilifuata ambapo yasemekana kuwa Bedbug alikuwa amerudi kwao nchini Uganda. Kingsting kiupande wake alifungua kampuni yake ya kuandaa matamasha kwa jina TAMASHA ENTERTAINMENT, vilevile aliendelea kufanya muziki ila ni baadhi ya vibao vichache tu vilivyovuma kama kibao SHEREHE. Juzijuzi Kingsting alitoa wimbo mkali kwa jina MOMBASANI SHWARI ulioandaliwa na video director ENOS OLIK wa Nairobi.Wimbo huo ambao kwa sasa unafanya vyema katika chati tofauti za muziki ulidhihirisha kuwa Kingsting anao uwezo kipekee. Katika mahojiano hapo jana ndani ya Baraka fm Kingsting alidokeza kuwa msanii mwenzake Bedbug amerudi tena na wapo tayari kuwaangushia burudani la kukata na shoka kama zamani. " Bedbug yupo Kenya na tayari tushaanza maandalizi na mipango kabambe ya kufanya kazi pamoja kama vile zamani." alieleza Kingsting. Japo kuwa hakusema wakati upi watakapo wachilia vibao vyao, tunasubiri kwa shauku kuu comeback yao.
Comments
Post a Comment