THESE ARE MY CONFESSIONS! EVE WA NZUMARI AONGELEA YOTE YANAYOMHUSU!!!
Eve Queen Adhiambo mwanzilishi na mmiliki wa Nzumari awards ameamua kufunguka na kudokeza yote yanayomkumba waziwazi. Binti huyu ambaye ni mshika dau mkuu kwenye tasnia ya muziki wa pwani alinakili haya kwenye ukurasa wake wa facebook........."Hii barau na waandikia marafiki zangu wapenzi wa fb kuwaeleza mbivu na mbichi kunihusu, kwanza kabisa namshukuru Mola kwa maisha yangu na mapenzi tele alio nayo kwangu mimi, maisha ya Ustar inataka moyo tena uwe mtu usio ya sikiliza ya watu wanapo kunena vibaya, nilikuja kutana na my kaka Director#Billy Ogoda# alipokuja kunifanyia interview na baada ya hapo tulianzisha kipindi, alikua ameskia mengi kunihusu na kama wengi wenu alikua akiamini yote aliyo ya soma kwa magazeti kunihusu na chochote alicho kiskia kwa watu, baada ya kunijua kwa undani hapo basi ndo aliamini mengi yanayo andikwa na kusemwa kunihusu ni porojo, maisha ya Ustar inabidi kufanya mambo mengine ili upate kiki na uzidi kuongelewa ndo usipotee kwa midomo ama macho ya mafans, leo hii nawambia ukweli mtupu na mastar wote wanakijua inabidi saa zingine utunge story ili upate kuongelewa, mimi nilingia kwa showbiz nikiwa na umri wa miaka 19 na kuanzisha nzumari na miaka 22, na amini nina nyota nzuri ndo manake si ishwi kupigwa vita, mapicha ninayo post kwa fb hapa na mume yoyote hakuna ata mmoja nishawai kua na usiano wa ndani ya kimapenzi, kuna moja nilipost msichana aki kiss mwanamume na kudai ni mume wangu hio nilitoa kwa internet haikua mimi kabisa, na kusema kweli hio picha iliuza sana na nilipata kiki, uwa ina bidi kufanya hivyo ndo uwe kwa lugha ya kimombo rellevant, kama mnaweza kumbuka picha ya Nyota na Tunda man hizo pia zilikua sababu ya kiki, lakini nimegundua yote hayo ni upuzi mtupu sababu mimi ni mtoto wa kike na naji dhalilisha na tena nishakua mzazi, wengi wameni hukumu na wala sitawai walaumu kwa sababu nilisababisha mwenyewe, picha ya ukweli hapa ni mimi na babake mtoto wangu tu na issue ya Ordinareh Bingwa kama Mungu alipanga ni sawa kama hakupanga sitakufa moyo kumngoja wangu wa milele lakini kwa sasa nataka kuweka maisha yangu ya kimapenzi siri mpaka mtakapo ona nimevishwa pete, najua haitakua rahisi kwangu manake mimi nikipenda napenda na uwa sijali ata dunia nzima ikijua, mapenzi kikohozi hakifichiki lakini nitajaribu kadri ya uwezo wangu kuficha, wengi unitumia inbox wakiniambia mimi ni role model na nataka kuwapa mfano mzuri na sio kuwapotosha, mimi ni koo cha jamii na poleni sana kwa wale nilio wakosea heshima na niko tayari kurekebishwa ninapo kosa sababu hakuna alie kamili....nikimalizia sijawai kua na usiano wakimapenzi na Jaguar, Ommy dimpoz naapa leo juma pili kama nadanganya Ewe Mwenyezi Mungu ni laani#Eve Reborn# maturity comes with age# am not perfect#...........
Comments
Post a Comment