VIVONCE THE FLAGLADY AWAHIMIZA WASANII WA KIKE PWANI WAWE NA USHIRIKIANO.
Huku sanaa ya pwani ikiwa na wingi wa wanamuziki wa kiume na wachache mno wa kike,msanii Vivonce amejitokeza bayana na kuwaita pamoja wasanii wa kike ili wawe na umoja.Tukimsheherekea Nyota Ndogo kwa hatua kubwa aliyopiga kuiwakilisha pwani nchini USA kwa tamasha la muziki,Vivonce the flag lady amechoshwa na utengano ulio na madivas wa sanaa ya pwani.Msanii huyu ambaye hivi majuzi amevuma kwa kibao chake 'yelile' na 'the jembe' alioshirikishwa na kidis alinena haya kupitia ukurasa wake wa facebook na alionyesha uchungu na wivu kwa wasanii wa kiume jinsi wanavyoshirikiana na kufanya kazi pamoja huku mabinti wakitengana.Vivonce alikuwa na haya ya kunena...."Huwa naona UWIVU ninapowaona WASANII wa kiume Pwani wanapopeana Ushauri ama kuungana mikono kwa kazi zao na wanafanya kazi katika Studio tofauti ila wana ushirikiano wa ajabu!! nimetunuku sana... Sijawai hata kuskia ama kuona kwa Wasanii wa KIKE pengine ndiyo maana kunapokuwa na sherehe yoyote mkoani Pwani unaona kwa POSTA wasanii wa kiume kibao tena WENGI na wakike ni mmoja tu na tupo wengi tu tunaofanya vyema hivi unaona SHIDA ikowapi?
Comments
Post a Comment