TED JOSIAH AJITOLEA KUFANYA KAZI NA UPCOMING ARTISTES DAIMA NA HAIGOPI KAMWE!!
Wengi wanamfahamu kama pioneer wa muziki wa Kenya na vilevile
ukimuita legend hutakua hujakosea.Tunamzungumzia produza gwiji na
shupavu Ted Josiah.Produza huyu amerudi chini kabisa kutafuta talanta
changa na mpya ili kuweza kuzikuza.Huku akiwa na sifa kemkem za kuwatoa
wasanii gwiji kama Gidigidi Majimaji,Wyre,Nazizi,Prezzo na wengine
wengi.Ted amekiri ya kwamba daima atafanya kazi na wasanii wanaochipuka
wa hapa Kenya hadi wapate mafanikio.Tukimnukuu kupitia ukurasa wake wa
facebook,Josiah alinakili haya......"I am not ashamed to get my hands
dirty, to be laughed at when i am down in the trenches helping new
talent come to the front. I am proud to be Kenyan and will make sure our
Kenyan talent becomes as big as any talent anywhere in the world. Lets
start being very proud of who we are.
I AM LOUD PROUD AND KENYAN" Huku akiyanena haya,produza huyu
amedhihirisha bidii yake ya kukuza sanaa kwani tayari amewasajili
wasanii Hustla-Jay na Iddi Hemedi wanaotokea hapa pwani.Tayari wasanii
washatoa video kalikali zikiwemo Continental Scar ya Hustla-Jay na
Usijali ya Iddi Hemedi.
Comments
Post a Comment