KIDIS APATWA NA TETESI HUKU AKIJITAYARISHA KWA KIBAO KIPYA.
Huku akijivunia mavuno yake ya wimbo 'Kamua leo remix' msanii Nesphory Simbiga almaarufu Kidis amekumbwa na tetesi zinazovuma kwenye magazeti ya kuwa ameyasahau majukumu ya ulezi.Kidis ambaye kamwe amekimya kwa tetesi hizi,lengo lake kuu ni kuhifadhi heshima na hadhi kama msanii anayeheshimika kwa jamii tofauti.Kulingana na utafiti wetu,Kidis amejaribu kunena yanayomsibu kupitia wimbo wake 'The Jembe' aliomshirikisha Vivonce.Vilevile,msanii huyu japokuwa anakumbwa na uvumi,propaganda na tetesi hizi bado yupo imara na ameonyesha bidii zaidi pale alipotangaza wazi kuwa yupo kwenye maandalizi au tayari ameshaanda wimbo akishirikiana na msanii wa kimataifa STL.
Comments
Post a Comment